Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiagana na Msaidizi Mkuu wa Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Derhan Dogan katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam leo, wakati Makamu wa Rais alipokuwa akielekea Nchini Uturuki kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa nne wa Umoja wa Mataifa, utakaozungumzia juu ya Maendeleo ya Nchi masikini Duniani. Mkutano huo unatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo mjini Istanbul. Katikati Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Mahadhi Juma Maalim. Picha na Amour Nassor VPO
Home
Unlabelled
Makamu wa Rais aenda uturuki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...