Waziri wa Ujenzi Dr . John Magufuli (mwenye pama) akiangalia vifaa vya ujenzi katika bohari ya Kampuni ya ujenzi ya Kharafi kutoka Kuwait vinavyotumika kujengea kipande cha kilo meta 60 kutoka eneo la Ndundu-Somanga mkoani Pwani. Mwenye shati la Mandela ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Bw. John Ndunguru.
Waziri wa Ujenzi Dr . John Magufuli akiangalia vifaa vya
ujenzi katika bohari ya Kampuni ya ujenzi ya Kharafi
Waziri wa Ujenzi Dr . John Magufuli (mwenye pama) akivishangaa vifaa vya ujenzi katika bohari ya Kampuni ya ujenzi ya Kharafi kutoka Kuwait vinavyotumika kujengea kipande cha kilo meta 60 kutoka eneo la Ndundu-Somanga mkoani Pwani. Pembeni yake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Bw. John Ndunguru.
Waziri wa Ujenzi Dr , John Magufuli akikagua ujenzi wa eneo la kipande cha kilo meta 60 cha uwekekaji lami cha Ndundu- Somanga kinachojengwa na Kampuni ya Kharafi kutoka Kuweit
Sehemu ya barabara ya Kilwa road ambayo Waziri wa Ujenzi Dr. John Magufuli Mei ameikataa kutokana na kujengwa kwa kiwango cha chini.
Waziri Magufuli (kushoto) akiongea na watendaji wake pamoja na mkandarasi wa barabara ya Kilwa road jijini Dar ambapo alikataa kuipokea kwa kuwa na kiwango cha chini. Picha zote na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO


Tusaidie Mheshimiwa Magufuli, maana tokea kilometa 60 imeanza kutengenezwa huu mwaka wa ngapi sijui. Panachosha sana hapo.....
ReplyDeleteTanzania bwana miaka mingapi ndio leo Magufuli anaanza kulalamika?
ReplyDeleteSWALI kwani enginer wa tz hawapo mpaka barabara karibu inaisha ndio waanze kulalamika?
HADITHI HADITHI ZA BIBI YANGU usiksalie kinu utaoa maishani
magufuli nakufagilia sana ,hebu ondoa kero pale mbagala rangi tatu maana watumiaji wa barabara hiyo wanahangaika sana na kipande hicho
ReplyDeleteNa sisi wabongo tuwache kuiba vifaa vya ujenzi. Niliwahi kumsikia Engineer wa barabara ya Kilwa akilalamikia wizi wa vifaa kwenye tv. Sasa munadhani yeye atatoa wapi vifaa vya ziada wakati na asilimia kumi tumeshachukuwa?
ReplyDeletehii nchi inataka mtu mmoja ambaye hacheki na watu,mambo ya kishenzi shenzi yote yanatakiwa watu waadhibiwe...watanzania hawana nidhamu hata kidogo nakumbuka mzee mkapa amefungua uwanja wa taifa siku hiyo hiyo watu wamekunya kwenye masinki ya kuoshe mikono sasa hawa watu gani...dawa sio kucheka na watu kabisa.
ReplyDeletemagufuli nakukubali mfuatiliaji makini ndio maana ujenzi wa barabara ya Jet Lumo hadi Davis corner unaanza kushika kasi, lakini tunaomba utusaidie na sisi tunaotumia sehemu ambayo mkandarasi hajaifikia kuanzia Abiola hadi Davis corner kwa kuwa kuna madimbwi na mashimo makubwa aikarabati ili iweze kupitika. Hivi sasa sehemu hiyo inapitika kwa tabu na hivyo kufanya nauli za daladala kupanda hadi kufikia sh. 500 na pia wenye magari madogo hawapiti kabisa
ReplyDeletewatanzania sisi ustaarabu hatuna kabisa, huwa tunaona kama tunamkomoa mtu kumbe tunajirudisha nyuma kiamendeleo. Unaiba kitendea kazi kwa njaa ya siku moka wakati barabara hiyo itakupa ridhiki ya miaka nenda rudi wewe na ndugu zako wote na familia yako.
ReplyDeleteHebu sijui nani aje atupe darasa la ustaarabu, ustaarabu umetushinda kabisa sisi Watanzania, ndio maana tuna kila kitu lakini ni maskiiniii wa kutupwa, SHAME ON USSSSSSS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Two words. Barabara Ijengwe.
ReplyDeleteBig up Magufuli! Sasa tungojee waende kukustopishia mikoani
ReplyDelete