Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mizingani Wambaa, yenye urefu wa Kilometa 9.7 kutoka kwa Injinia Gaitano Musuku, (kushoto kwake) wakati alipotembelea na kukagua akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba leo Mei 18. Kushoto ni Ofisa msimamizi kutoka Wizara yaMaswasiliano na Miundombinu Zanzibar, Hamadi Baucha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiangalia maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mizingani Wambaa, yenye urefu wa Kilometa 9.7 inayoendelea kujengwa, wakati alipotembelea na kukagua akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba leo Mei 18. Kushoto ni Ofisa msimamizi kutoka Wizara yaMaswasiliano na Miundombinu Zanzibar, Hamadi Baucha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimbini iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akiwaaga baada ya kuweka jiwe la Msingi katika shule hiyo leo Mei 18, akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba.
Wanafunzi wa Kidato cha pili katika shule ya Sekondari Kangani iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, Siti Said Ali (kushoto) na Feda Ali Othman, wakiimba utenzi wenye ujumbe ikiwa ni sehemu ya burudani wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, alipofika Shule ya Msingi Mjimbini kuweka jiwe la Msingi leo Mei 18.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...