Home
Unlabelled
formal dinner setting...kwa wasiojua
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Tuondoleeni za kitumwatumwa hapa. "forma" dinner setting- according to who?
ReplyDeleteTandika mkeka chini, lete ugali/wali/matoke; n.k pitisha maji ya kunawa. Hii ndiyo "forma" dinner setting ya tulio wengi wetu Africa. Hii tabia ya kujifanya mmevizoea vitu visivyokuwa vyenu pelekeni mbele ya safari huko.
Huyu jamaa ametuletea Dinner Setting ya Kimaarekani. Watanzania tuna aina yetu tofauti kabisa ya dinner. Hizo Salad kwetu zinapikwa kama mboga, halafu hiyo Dessert Fork ya nini wakati sisi baada ya kula tunakuwa na ndizi, embe au machungwa pembeni. Mtu asikusimulie, diet ya kiafrika poa sana.
ReplyDeleteWewe Ndio umegunduwa leo nini endelea tu kama kina sie na mkono Ugali inatosha wacha kujiumiza mila za watu ndio mwanzo unachika kikombe cha chai mwanaume vidole viwili. MZ.
ReplyDeleteGlass zote hizo zanini wakati glass moja tu inatosha? Mlo wa kitanzania hauna supu!!
ReplyDeleteaah wapi. mbona sioni maji ya kunawa?
ReplyDeletekwetu hata ukiwa unatumia kijiko(yeah hatujui kutumia umma na kisu) lazima pawe na bakuli la maji ya kunawa.
Mambo ya kuendekeza ulaya-laya ndo haya.Hakuna mwenye na pride na uafrika anymore.So sad.
Jamani ndugu zangu wooote mliotoa maoni hapo juu nawashukuru kwa kuupenda utamaduni wetu kuliko kuiga vya wenzetu. Lakini dunia imekuwa ya utandawazi. Leo utataka uende marekani, ulaya au australia. Huko utakutana na hayo maglass, nyuma, mavisu mengi na masahani yake. Sas kama hukuvizoea vitakuaibisha. Kwa hiyo mshukuruni jamaa aliyewawekea hapo ili mpate funzo kidogo. Hata kama hatupendi mila za watu lakini kuzijua si dhambi. Vilevile watakapokuja kwetu kutalii wengine wangependa muwakirimu kwa tamaduni zao vinginevyo hawatakuja tena. Ukizingatia wametupiga bao kwa kila kitu. Ni mambo managapi tumewaiga? karibia kila kitu ni cha kwao. Hongera sana mdau kuweka vitu kama hivyo.
ReplyDeletemdau ul ilietoa fomal dinner nakuunga mkono.elimu haina mwisho,na ziada sio mbaya ila kipigo.
ReplyDeletesasa kuna ubaya gani kama mtu anafahamu kitu halafu akaamua kukitoa katika blog ya jamii ili kuelimisha.
jamani tanzania yetu ni kubwa sana nasi tuko watu wa aina nyingi mno na hari tofauti sana,kumbuka kuna watu bado hata vyoo hawajaanza kutumia bado wako na majembe ya kuchimbia punde wawapo na haja.kuna watu hata ustaarabu mdogo kabisa hawaujui,mtu anaweza akakukanyaga bahati mbaya na akakupita bila kusema samahani,kwenye mabasi bado tunakimbizana kukimbilia kupanda kitu ambacho kamatutatumia ustaarabu kidogo wa kupanga mstari sote tunaweza kupanda.
kwa mtazamo wangu mimi nadhani tusikatetamaa tuendelee kuelimishana.nafahamu utamaduni wetu ni mzuri sana and im proud off.ila sitochoka kujifunza lolote linaloweza kunielimisha kwani sitopata hasara ila nitafaidika zaidi.
akhsanteni.
mdau washington
Anon wa 06:38, watu tuko huko miaka Mingi, na tuna hudhuria hayo unayoita formal dinner mara nyingi, lakini unakula kwa kijiko, na Nyama na Mikate unakula tu kwa mkono kama kawaida, tena wa kulia, hakuna anayejali. Utakuta wakuja kama wewe mnahangaika na umma mkono wa kushoto, kisu kulia.... Kaazi kwelikweli, na mnaacha chakula huku njaa zinawauma!, Eti kuwaonyesha na ninyi mnajua!
ReplyDeleteAsingeita "Formal Dinner Setting", bali angeita tu "Western Dinner Setting" tusingekuwa na bifu. Halafu ameboa zaidi aliposema "Kwa wasiojua"....ebo, kwani lazima?!!
ReplyDeleteAsante mchangiaji wa sita,watanzania bwana ndio maana hamuendelei yaani ni sawa na kusema mimi sitengenezi bara bara kwa kuwa zilianza kutengenezwa ulaya no wonder mpaka leo mnalala kwenye ngozi ya ng'ombe na nyumba za tembe shenzi zenu...mtu mzima anadiriki kusema siendi hospital kuna dawa za wazungu so niende kwa babu..pumbavu........zenu,africa maendeleo mtayasikia kwenye radio na sijui kama mtayasikia kweli maana hata radio zenyewe hamna....mnataka utandawazi, siku hizi dunia ni kijiji mnatakiwa ku integrate mila na watu wengine ili kuleta maendeleo,mambo ya kula na mikono matokeo yake kipindu pindu hakiishi maana watanzania hata mikono hawanawi wakitoka chooni, mnaletewa fork,vijiko na visu mnadai ni uzungu haya kaeni na uafrica wenu wenzenu wanapiga hatua mbele kwa mbele.
ReplyDeleteFormal, academic, conventional may have either favorable or unfavorable implications. Formal may mean in proper form, or may imply excessive emphasis on empty form. In the favorable sense, academic applies to scholars or higher institutions of learning; it may, however, imply slavish conformance to mere rules, or to belief in impractical theories. Conventional, in a favorable sense, applies to desirable conformity with accepted conventions or customs; but it more often is applied to arbitrary, forced, or meaningless conformity.
ReplyDeleteUkisoma sentence ya mwisho insema kama ni desturi za kitumwa.
Kwa hiyo unaposema formal, unamaanisha to who? Kaka michuzi usitoe vitu kwenye google ukavi-impose kwenye society yetu..ndio maana maadili yanapungua kwa ajili ya kugeza.Who cares about formal dinner setting, kwanza ukitaka ule undani kabisi, this also depends on the menu...kwa hiyo, hiyo pekee can not be formal. What if am having oysters for starters will the setting surfice. Jamani give us a break.
Mhhh mi nawashangaa sana wabongo, tena mnchekesha mbona mnaiga mambo mengi ya kila siku... jitazame mwenyewe toka asubuhi unavyo amka hadi usiku unapokwenda kulala, hivyo yote ufanyayo ni ya kiafrika au kiTanzania? hayo ni mawazo mgando... heki bongo flava wanafanya nini? cheki maofisini wanavaa nini, cheki picah za kanda za watanzania wanafanya nini?
ReplyDeleteEbu nenda mgahawa wowote hapa bongo, nasiku hizi wabongo wanapenda kwenda migahawa ya kigeni, kaa pembeni angalia jamaa anavyo hangaika na hivyo visu, uma vijiko, uma mkono wa kulia kisu mkono wa kushoto sasa utakata vipi kwa kumia mkono wa kushoto? mtu anakula huku anaongea chakula kinamtoka mdomoni, mhh kazi kweli kweli, mtu anakula kwa kutukia uma mkono wa kulia, kisu mkono wa kushoto huku anaongea kwa jazba maongezi yakikolea basi kile kisu kipo juu kwa juu kinazungunguka..... saa jamni mliotoa maoni ya kashfa hapo juu, naona hamna mpango wa kugombea nafasi za juu ngazi ya uongozi? Duh ndigu zangu, kujifunza sio kuharibu bali ni faida kila kitu kina uzuri wake na ubaya wake.... wazungu nao wakija kwetu hasa wanaokwenda vijijini wanapenda kula kwa mkono.... ebu wekeni mtazamo sawasawa...
Hivi wabongo mbona tunapenda kuwa watu wa Critisize tuu. Mini ni mafanyakazi wa serikali tena mtoto wa Mkulima tuu sijui. Lakina kwa proffession yangu na kazi ninazofanya nimekuwa ni mtu wa kusafiri kwenda nchi za watu mara nyingi tuu nma sio siri safari zangu zote za kwanza nilichemsha kupita maelezo kuhusiana na suala zima la mambo hayo hapo juu. Nakushukuru mdau kwa kulileta hili kwa mtu yeyote mwenye akili timamu amekuelewa.Ikumbukwe kwamba kujifunza vitu hakuna mwisho. unajua nini unaweza kumjaji mtu Kutokana na maneno anayoyaongea kwa hiyo siwashangai hao wadau wa kwanza kutoa maoni ni sawasawa na yule mbunge aliyesema basi tufunge mlango tupigane hivi nani alitegemea maneno yale yangetoka kwa kiongozi kama huyo aliyechaguliwa kwa kura za wananchi kibao. Hongera mdau I NEEDED THAT.
ReplyDeleteAngali filamu inaitwa "Pretty Woman", itakuonyesha kuwa hiyo "formal dinner set" wazungu wenyewe wa Ughaibuni haitumii majumbani kwao. Mwisho wake ni mahotelini. Hata hapa Tanzania ukienda mahotelini ndio utakuta hayo mambo. Kujua dinner set hakumsaidii Mlala Hoi kujikwamua na umasikini wake.
ReplyDeletewatu waliomkandia mtoa maoni ya awali ni wakushangaza na inabidi kujifunza. Huyu bwana alichodhamiria sio kuwa tule hivyo majumbani mwetu Bongo, ni pale mtu kasafiri kikazi, Ulaya au wageni wa ulaya wamekuja kututemebeal, sema kiserikali au kampuni zetu za kigeni au kivingine. huo mpangilio utaukuta tu kwenye dinner, na hakuna mkeka. Tunapooana watu mbali mbali wameenda seminaa, kozi fupi hata zile za umoja wa afrika mashariki, mambo ni kama hivyo, hata ugali unawekewa umma. acheni mawazo ya kimaskini, tamaduni tunajifunza zote..
ReplyDeletemnakumbuka soga la kawawa, kuwa kawekewaa chai hadi kataka kufa hadi mchinga kamwabia, rahsidi funika kikombe, watakua.."
osheni vinywa kama umezoea kula manzese kwa mfuga mbwa, lakini nenda ubungo plaza au mwenge ambako mtu anategema wageni mbali mbali wakiwemo wamatumbi, basi utaratibu ni huo..na habari ndio hiyo.
Michuzi tunakakuhsuuru.
mdau, Ulaya
Tuwe wakweli.......mbona tunatumia karatasi za chooni......hata kwenda na kopo msalani bila kutumia jiwe au majani? hata Mchanga! Mbona tunatumia dawa ya mswaki badala ya mkaa.........! Kama tumecopy na kupaste mengine kwa vipi hili liwe shida? Wengi hapa ni kina Juma au John, Halima au Anna.....hata imani za Muumba tumekopy na Kupaste! Hebu tukubali ukweli tumefungwa goli na watu wenye rangi nyeupe! Angalia Komputa unayotumia....angalia kiyoyozi kinachonipulizia.....angalia Umeme........angalia tiles.....Kalamu nayotumia......Calculator......Mobile phone.....!licha ya mkoko wa Ford.....Toyota......Maruti.......Benzi!Sembuse tuogope kufundishwa kula kistaarabu........Sipendi kula chini mkekani! Wote kwenye sahani moja.......wenye ukoma......safura....... wote tunachovya sahani moja! Ya nini taabu yote hiyo..... kula inakuwa adhabu au karaha....!Asante michuzi kutupa somo! Babu yangu aliniambia Ukweli......Baada ya Muumba Mwenyezi Mungu.....ndio tukaja watu weusi! UKWELI UNAUMA LAKINI UNAPONYA!
ReplyDeleteUNACHEKESHA NDUGU YANGU AU UMECHEMSHA HUNA JIPYA KABISAAAAAAAAAA
ReplyDeleteNia na madhumuni ni kwa wanaouona umuhimu na hawajali kufumbua macho zaidi (mimi boi na hayo ndiyo tunayosomea)ni kwa waliotaka kufahamu zaidi. Kama wewe umeridhika na hali - basi ni muafaka na ni vizuri usiingie kwenye mdahalo ambao haujengi chochote. Kwani unapojiita mstaarabu ni kwa vipimo vipi? Unapovaa nguo za pamba wakati wa joto na za sufi wakati baridi? n.k. Dunia nzima tunajifunza yale mazuri toka kwa jirani au wenzetu.
ReplyDeleteJamaa anajaribu kujibu mapigo umechemsha jaribu tena baadae hahahaha!
ReplyDelete