SIMBA v WYDAD CASABLANCA
Mechi ya kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kuondolewa kwa kuchezesha mchezaji asiyestahili imepangwa kufanyika kati ya Mei 27, 28 na 29 mwaka huu kwenye uwanja huru (neutral ground).
Simba ya Tanzania na Wydad de Casablanca ya Morocco ndizo zitakazopambana katika mechi hiyo ya mkondo mmoja.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) linatarajia kutaja katika muda mfupi ujao nchi ambapo mechi hiyo itachezwa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) linatarajia kutaja katika muda mfupi ujao nchi ambapo mechi hiyo itachezwa.
Timu itakayoshinda itaingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, ikiwa kundi B pamoja na Al Ahly ya Misri, Esperence (Tunisia) na Moloudia Club d’Alger ya Algeria.
Timu itakayoshindwa itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya
Timu itakayoshindwa itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya
Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya kwanza nyumbani na Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.
MAPATO STARS v BAFANA BAFANA
Pambano la kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Afrika Kusini (Bafana
Bafana) lililochezwa Mei 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 75,888,000 kutokana na watazamaji 10,554 walionunua tiketi.
Watazamaji 240 walilipa sh. 30,000, 585 (sh. 20,000) na 1,423 (sh. 10,000), 614 (sh. 7,000) na 7,692 (sh. 5,000).
Watazamaji 240 walilipa sh. 30,000, 585 (sh. 20,000) na 1,423 (sh. 10,000), 614 (sh. 7,000) na 7,692 (sh. 5,000).
Baada ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 11,576,135.59 na gharama za awali za mchezo ambazo ni sh. 21,843,600.00 mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 10 kwa uwanja sh. 4,246,826.44, asilimia 10 kwa gharama za mchezo sh. 4,246,826.44, asilimia 5 kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 2,123,413.22 na asilimia 75 kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 31,851,198.31.
Nacho Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata asilimia tano kutoka kwa mgawo wa TFF ambayo ni sh. 1,592,559.92.
SEMINA YA WAAMUZI WA FIFA
Semina kwa waamuzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Dar es Salaam kuanzia Mei 17 hadi 19 mwaka huu.
Wakufunzi wa semina hiyo ni Riziki Majalla, Leslie Liunda na Omari Kasinde.
Wakufunzi wa semina hiyo ni Riziki Majalla, Leslie Liunda na Omari Kasinde.
Waamuzi hao ni Ramadhan Ibada, Waziri Sheha, Oden Mbaga, Judith Gamba na Israel Mujuni.
Waamuzi wasaidizi ni Hamis Chang’walu, Ally Kombo, Saada Tibabimale,
Waamuzi wasaidizi ni Hamis Chang’walu, Ally Kombo, Saada Tibabimale,
Josephat Bulali, Samuel Mpenzu, Erasmo Jesse, Mwanahija Makame, John Kanyenye na Khamis Maswa.
Imetolewa na Boniface Wambura
Afisa Habari TFF
sikutegemea umati mdogo kiasi kile. nadhani TFF waache kuwabana wananchi. hali ya sasa ni ngumu kwa individual citizens. kwa hiyo kuweka kiwango cha 5,000/= kwa makabwela katika mechi ile isiyo ya kimashindano haikuwa sahihi. TFF ijue kuwa uwanja ule unapaswa kujaa kila taifa linapocheza, hasa kwa mechi zinazooneshwa na vituo vya kimataifa, kwani hii inasaidia kuitangaza nchi yetu, utalii na wachezaji pia. lakini kwa uchache wa namna ile wa kulaumiwa ni Wizara ya Michezo na TFF. kwa Mtanzania wa kawaida lazima ataingia gharama nyingine hadi kuingia uwanjani, mathalani anakaa Kibaha. piga hesabu ya haraka haraka gharama anazoingia uwanjani. lakini ukimwekea kiingilio cha 3,000/= angalau kinamvutia kuingia uwanjani. TFF mbadilike. najua si nyie pekee wenye maamuzi na uwanja huo, ilka mna uwezo mkubwa kuishawishi serikali katika hilo. tubadilike, nchi hii ni yetu wote
ReplyDeleteHao CAF wanawatafutia aibu simba. maana watakula kichapo kuliko kile cha TP Mazembe.
ReplyDeleteNyie wachezaji wa Stars inabidi mnatakiwa kushinda mechi hizi..tatizo siyo viingilio tu hata matokeo ya timu yanachangia watu kuipenda timu ya Taifa.Watu hawaezi kuwa wanalipa hela zao halafu mnafungwa 'kizembezembe'.Na kwa taarifa yenu hii mechi ilikuwa kwenye kalenda ya FIFA(angalia www.FIFA.com/worldfootball mtakuta mlivyopanga matokeo mabaya pamoja na yale ya msumbiji 2-0.
ReplyDeleteTatizo la foleni ya Magari nalo linachangia mahudhurio hafifu.Mfano watu wanaotumia Morogoro road zaidi ya Ubungo au Bagmy rd zaidi ya mwenge wanajiuliza mara mbili mbili kuja uwanjani.Kufika taabu,kurudi ndiyo usiseme.Nyie simba mmefanya nini sasa..hao si mmnafanya nao biashara fulani?leo mmewageuka..Mnawafahamu wacongo au mnawasikia?huo uhasama utakuwa zaisi ya huo mpira..utaenda mbali zaidi..(Mimi Simo)
D.Villa
Nashangaa timu zetu za Tanzania sisi tunajijuwa ni watu wa kushiriki tu katika mashindano lakini si kwa lolote,tuna uwezo gani hata tukathubutu kwenda kukata rufaa ya kuwa eti wamechezesha mchezaji sie hebu tujiangalieni na sisi jamani Tanzania?, sie kwa kusema tu hapo kweli tunaweza kuchukuwa kombe la aina yoyote kuna vitu vyengine tusijaribu kuwaharibia wanaojuwa jamani (Maoni)
ReplyDelete