Jane Miso

Katika tamasha la Iringa uzinduzi wa album ya kwanza ya muimbaji wa Muziki wa Injili ambaye alitamba katika muziki wa kidunia na kibao cha Riziki alichowashirikisha waimbaji kama Stara Thomas na Bizman ndugu K’Bazil atasindikizwa na waimbaji wadogo na wakubwa akiwemo muimbaji Jane Miso ambaye anatamba sana na nyimbo kama Omoyo, Motima, Uinuliwe Baba na Usikumbuke Uovu Wangu

Jane Miso ambaye hivi karibuni alifanya uzinduzi wa album yake ya UINULIWE chini ya Haak Neel Production amesema amefurahishwa na kupendezwa na K’Bazil kwa uamuzi wake wa kuokoka na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Kwa kumtia moyo na kumpa nguvu ya kusonga mbele amekubali kwa moyo mmoja na kumsindikiza K’Bazil katika uzinduzi huo.

Jane Miso atakuwepo katika tamasha hilo la kwanza la uzinduzi wa albam ya "Yesu Ananipenda" yaK’Bazil litakalofanyika mkoani Iringa mnamo tarehe 5 Juni ya 2011 na baadae kufanyika katika mikoa mingine tofauti nchini Tanzania.

K’Bazil amabaye pia ni mmoja kati ya wachungaji katika kanisa la Glory Of Christ ama Ufufuo Na Uzima lililopo Kawe, Dar es salaam ambalo hapo awali lilikua Ubungo, Chai Bora lililo chini ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima Album ya  kwanz aya Muziki wa Injili inakwenda kwa jina la “Yesu Ananipenda” Ina nyimbo 10 ambazo ni Namjua, Wakati Na Bahati, Wewe Ni Baba, Rudisha, Utukuzwe, Moyo, Asante Yesu, Tusonge Mbele, Mama na Yesu Ananipenda ndio nyimbo iliyobeba jina la album.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...