Afisa wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera PC Joseph akitoa mafunzo ya udereva kwa madereva toka maeneo mbalimbali yaliyoko wilayani Muleba, kikosi hicho kinatoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na chuo cha udereva cha Lake zone kilichokopo mkoani Kagera ambacho kimejizazititi kwa kutoa ushirikiano na jeshi la polisi katika juhudi za kupambana na ajali za barabarani
Mkurugenzi mkuu wa chuo cha Lake Zone Bw. Wiston Kabantega akiwaelezea madereva namna ya kujiepusha na ajali wakati wa mafunzo ya udereva yanayotolewa na jeshi la polisi mkoani Kagera kwa kushirikiana na chuo hicho yanayoendelea wilayani Muleba katika ukumbi wa Calfornia.
Mrajisi msaidizi mkoani Kagera Juma Mokili akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ushirika mkoani Kagera.
Inamuonyesha mwenyekiti wa chama cha ushirika mkoani kagera (KCU) john Binushu akitoa taarifa kwa wajumbe wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu ulioandaliwa na chama hicho ambao ulifanyika jana katika hoteli ya yassila uliokuwa mahsusi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mizania. Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii, Kagera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2011

    Hii ni habari nzuri, keep it up. Kazaneni kwa waendesha pikipiki pia. Maana huku Dar siku barabara za watembea kwa miguu na pikipiki hazijulikani wote tunakwepana humohumo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...