Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Dominique Strauss-Kahn (pichani), anatazamiwa kufikishwa mahakamani kufunguliwa mashitaka rasmi mjini New York baada ya polisi kumtia nguvuni kwa madai ya kujaribu kumbaka mwanamke mmoja katika hoteli mjini New York.

Wakili wa Bwana Strauss-Kahn anasema mkuu huyo wa IMF atakana mashitaka. Alikamatwa Jumamosi usiku akiwa ndani ya ndege ya shirika la Air France kwa safari ya kwenda Ufaransa. Polisi wanasema saa chache kabla ya hapo Strauss-Kahn alijaribu kumbaka mwanamke mmoja msafisha chumba katika hoteli ya Sofitel mjini New York.

Habari Kamili tembelea VOA Kiswahili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2011

    Maskini bosi wa IMF - naona alibanwa hadi uzalendo ukamshinda au siku za mwizi ni arobaini!! Ila jambo moja linafurahisha hapa ni kuona nchi zinazofuata sheria. Umetuhumiwa- hakuna cha bosi wa IMF wala IFM - utajitetea mbele ya pilato. ingekuwa nchi zetu ni nani amguse huyo!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2011

    sheria zingekuwa zinafuatwa bongo viongozi karibia WOTE wangekuwa ndani ama na kesi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 16, 2011

    jamani mahaba haina hela wala cheo, ukizidiwa ndio hiyo tena baba wa watu akajisahau! Alidhani kuwa mfagia chumba hata mpeleka mahakamani, Ulaya mambo ni tofauti. Tanzania wakubwa wangekuwa wanafanywa hivi, ufisadi ungeisha zamani, lakini tunaendelea kuwachagua na kutuumiza wananchi kila siku.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2011

    Haya hiyo ni tuhuma.lakini ni kweli au basi kama kawaida mabinti hawaoni aibu kuanzisha jambo ili mradi tu mtu anashushwa heshima yake.Binafsi ninaposikia habari kama hii hata siku moja sikurupuki kuhukumu.Sawa police wamepokea na kutekeleza,watafanya utafiti na haki itatendeka.nasema hivi kwa sababu tunaishi ktk ulimwengu ambao hauna uoga wa aina yeyote katika kuumba mambo.Wala sikatai kama mzee alipanda mori, very possible lakini yawezekana hata hakudiriki pia.Binti huenda anajua from now atakuwa maarufu,na dunia ndo hivyo ina kiu ya habari kila uchao.Ok Pole strauss.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 16, 2011

    Hamna, kitu hapo jamaa kafanyiwa zengwe tu na wapinzani wake. Eti niliingia chumbani kufanya usafi nilifikiri hayupo kumbe alikuwepo. Mtu yupo chumbani na hajacheck - out, unaenda kufanya nini chumbani. Hata hiyo hotel aliyofikia nina wasiwasi nayo, kinyume na hapo huyo boss pia angeweza kushtaki kwa kuingiliwa chumbani wakati akijiaanda, wala alikuwa hajarudisha funguo kwamba ametoka na mtu aje afanye usafi. So sio kushabikia tu, ni vizuri tukaangalia suala hili kwa mapana na marefu. Kwa akili ya kawaida na km unakaa sana kwenye mahoteli hii complain ya huyo mfagizi ina utata. Mfano mimi nipo bafuni naoga, nikimaliza sitafunga taulo wakati najiandaa, maana nipo peke yangu, sasa km wewe ulitegemea sipo, ukaingia bila kuuliza reception km nimetoka au la, ukanikuta nipo uchi ukataharuki nami nikataharuki nimeingiliwa nikataka kukuconfront kwa kukuuliza kwa nini umeingia bila ruhusa, ukakimbia, ukadhani nataka kukubaka, its complicated, ni mfano.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 16, 2011

    "ukanikuta nipo uchi ukataharuki nami nikataharuki nimeingiliwa nikataka kukuconfront kwa kukuuliza kwa nini umeingia bila ruhusa..." jamani hii ni attitude tu ya kutetea maovu na ndio hivyo hivyo tumeishia kutetea ufisadi kila uchao kwa vile wanaotuhumiwa ni 'wateule'. Kama hayo unayofikiria ndio yaliyotokea basi kwa nini usifikirie kwa nini huyo 'mteule' hakuripoti utovu huo wa nidhamu wa housekeeper kwa uongozi wa hoteli, lakini badala yake kachomoka mbio kiasi cha kusahau simu yake chumbani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 16, 2011

    Hiyi inawezekana imetungwa ili kummaliza jamaa kwa sababu inasadikika mwakani anaweza kugombea uraisi nchini kwake ufaransa na mchakato mzima unamuendea vizuri kwenye chama chake kisosialisiti.Inawezekana kafanya au ndiyo hivyo wanataka kummaliza,lote kati ya hayo yanawezekana

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 16, 2011

    Hii si mara ya kwanza bwana huyu kukuta na masaibu ya wanawake......ingawa sasa ni kwa jinsi nyingine.....!Tuna mengi ya kujifunza.....kama wadau walivyosema kwa mtindo kama huu bongo ingelifunga wanaume wengi, kuanzia viongozi wakuu hadi wasukuma mikokoteni.....!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 16, 2011

    Ingekua Mara moja ningekubali hiyo theory ya kumwangusha. Lakini watu wanajitokeza kila Mona as hivi na huko Kwao wanasema ndio mchezo wake. Aligusa pabaya this time au walimtumia maid mzuri ili amloge wamshike. Monica luinski remember? Usicheze na siasa nchi za watu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...