
Bi Janeth Kalinga (katikati) na mumewe Bw Brown Mbigili wakiongea na Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Elly Mwakyoma muda mfupi kabla ya kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi.
Janeth Kalinga, ambaye ni Katibu Muhtasi katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameelekea nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kupata ajali ya kuungua kwa moto mwezi August 2010 akiwa nyumbani kwake. Janeth alilazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kupatiwa matibabu ya awali. Amepelekwa India kwa matibabu zaidi ambayo yatagharamiwa na Serikali. Janeth ameishukuru Serikali pamoja na Wizara yake kwa msaada huo wa matibabu zaidi. Picha na Mwanakombo Jumaa
Pole mama yetu mpendwa!. Mwenyezi Munguy akutangulie na hata utakapokuwa huko India ukaweze kupata matibau sahihi na ukapate kupona haraka!
ReplyDeleteMdau
Pole sana dada Janeth Mungu atakuponya na maumivu uliyoyapata. Pia asante sana serikali kwa kuliona hilo kumpeleka dada janeth nje ya nchi kwa ajili ya matibabu zaidi, nawapa big up uongozi wote wa Wizara ya Habari, Vijana na Utmaduni na Michezo kwa kufikia maamuzi hayo mazuri kwa kumtibia Katibu Muhtasi nje ya nchi na hii iwe mfano katiaka Mawizara na Taasisi zingine za Serikali na hata binafusi.
ReplyDeleteabbie
Wee hapo juu unawaambia serikali na taasisi zingine ziwe zinapeleka watu nje badala ya kusema tunaomba serikali ijitahidi katika kuwekeza kwenye upande wa afya na afya za wananchi wote ujumla kwa kuweka huduma hizi muhimu nyumbani. Tunahitaji hospital zenye kuweza kufanya mambo mengi ili hiyo hela itumike hapa hapa kwetu. Kumbuka kuna watu wengi wanahitaji matibabu kama yake lakini hawana uwezo wa kwenda India na kama hufanyi kazi huko basi ndio hivyo Loliondo here we come.
ReplyDeletePole sana dada Janeth, Mungu atakusaidia upone kupitia matabibu. Hongera pia Mama E. A. Mwakyoma na Menejimenti ya Wizara ya Habari kwa kujali watumishi. Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na Ofisi nyingine zote za Serikali.
ReplyDeletesandag
ASANTE ANON WA 04MAY 11:03. POLE MAMA MUNGU AKUAAFU
ReplyDelete