Mstahiki Meya wa wilaya ya Temeke (kulia) Maabad Hoja akiingia katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za manispaa ya Temeke kwa ajili ya kuanza kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika leo.
Baadhi ya madiwani wa wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa umakini majibu ya maswali yaliyokuwa yanajibiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Eng.Gaston Gasama (hayupo pichani) wakati wa kikao chao kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo manispaa ya Temeke.
Baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wa wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa umakini majibu ya maswali yaliyokuwa yanajibiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Eng.Gaston Gasama wakati wa kikao chao kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo manispaa ya Temeke.
Madiwani wa wilaya ya Temeke wakiwa katika kikao chao leo kinachofanyika kila baada ya miezi katika ukumbi wa mikutano uliopo manispaa ya Temeke.Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Na Magreth Kinabo – Maelezo

Shilingi bilioni 2.5 zimetumika kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi 313 kati ya 427 kwenye mradi wa upimaji viwanja Gezaulole wilayani Temeke.

Hayo yamesemwa leo na ofisa mipango miji wa manispaa ya Temeke Photidas Kagimbo wakati akitoa taarifa ya maendeo ya mradi huo katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo.

“Zoezi hili linaendelea vizuri hadi kufikia jana tumeshalipa fidia ya shilingi bilioni 2.5 kati ya shilingi bilioni 2.8 zinazotakiwa kulipwa fidia kwa wananchi hao ambao ni sawa na asilimia 79,” alisema Kagimbo.

Aliendelea kusema kuwa maradi huo ambao ni wa awamu ya kwanza unajumla ya viwanja zaidi ya 700 na tayari zoezi la uchukuaji fomu limeshakamilika jana ambapo urudishwaji wake mwisho ni ijumaa ya tarehe 3 mwezi wa sita mwaka huu.

Kagimbo alifafanua kuwa mradi wa awamu ya pili uko katika mchakato na tayari fedha za fidia za kuwalipa wananchi zimeshatengwa ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni sita.

Alisema, “Kabla ya kufikia mwishoni mwa mwaka huu tunatarajia kupima viwanja zaidi ya 4000 katika eneo la Gezaulole na mara baada ya kukamilika kwa zoezi hili tutawajulisha wananchi ili waweze kutuma maombi kwajili ya kupatiwa viwanja.”

Mradi huu ulianza mwaka 2007 lakini ulisimama kutokana na ufinyu wa bajeti kwa ajili ya upimaji na ulipaji wa fidia kwa wananchi hivi sasa mradi huo unaendelea baada ya manispaa hiyo kupata fedha za mkopo kutoka Benki ya Rasilimali (TIB) na wizara ya Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nimekuona Waziri Kombo
    Longtime kaka
    Shavu kubwaaaaaaaaaaaaa
    God bless you man

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2011

    kaka michuzi tunaomba msaada. hivi gezaulole iko wapi. nasikia iko kigamboni lakini tukiangalia kwenye google map ya kigamboni haionekani. google map ya kigamboni iko shallow sana. i hope wazee wa temeke watashuhulikia hilo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2011

    zoezi la kuchukua fomu lilianza jumatatu, lakini fomu zote ziliisha siku hiyo hiyo ya jumatatu waliokwenda jumanne mimi nikiwa mmojawapo, tokea alfajiri saa 11.30 mpaka walipofika ofisini watendaji wa manispaa walitutangazia kwamba fomu zilimalizika tokea jana. Watu walishangaa sana. Lakini taarifa tulizopata katika mkanganyiko huo zilidokeza kwamba kuna watu wanachukua fomu 30 mpaka 50 kwa mtu mmoja. Sasa sijui utaratibu ulikuwaje, lakini sisi tulioathirika tulikasirika sana. Yalishawahi kunikuta kule Bunju, wale watendaje wa ofisi ya ramani walihodhi viwanja vingi sana kule Bunju kiasi watu wengi walikosa baadani tulikuwa watu wa kwanza kabisa lakini tukashindwa. Wanapokuja kuweka ile ramani ili uchague basi utakuta sehemu kubwa na nzuri wamechukua wenyewe na/au jamaa zao. Hio ndio hali halisi. Ndugu yangu Tibaijuka upo. Kazi kweli kweli hawa watu wako wameshakua sugu. Huu ni wakati wa kuneemeka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...