Nipo safarini huku Newala na hili ni eneo linaloitwa kitangari,lipo wilaya ya Newala,ni kilometa 30 kutoka eneo linaloitwa Mtama barabara kuu ya lami itokayo lindi kwenda masasi.Leo niliweza mwenyewe kuongea na bibi huyo hapo pichani anaeitwa Luwungi,nikamuhoji kuwa ilikuwakuwaje,akanambia kuwa alipata habari hizo ndotoni na kwamba moyoni mwake alisikia sauti ikimwamba awape watu dawa hiyo.
Pia bibi huyo anasema alipata kuanza shughuli hii tangu tarehe 6 mwezi April mwaka huu.hakuna tofauti sana katika ugawaji dawa kama kule semunge,loliondo.
Nimeona msururu mrefu wa watu wakisubiri dawa hiyo ambayo inasemekana kutibu magonjwa ya kifua kikuu,ukimwi na mengineyo sugu kama arobaini kwa ujumla wake.
ni hayo tu kaka kwa leo
mdau Hussein safarini Newala.


Eh! Mbona naona kama bibi ana maandazi pembeni(Picha ya kwanza)? Au hicho kikombe unasukumia na andazi ili dawa ifanye kazi ipasavyo?
ReplyDeleteIkiwa watu wengi namna hii, maana yake hata dawa inatibu. "Clinical trial" safi kabisa hiyo wasomi wa Muhimbili na UDOM na Kariuki. Taarifa za wanasayansi wetu walioifanyia utafiti dawa ya Babu ni kuwa inatibu hayo magonjwa sugu. Sasa kilichobaki mgariga upandwe nchi nzima.
ReplyDeletePatamu hapo yule wa sumange atakwambia yeye ndio anayemilki
ReplyDeleteNamshukuru mungu tumepata kikombe cha kwetu, maana ilikuwa ni ngumu kusafiri kutoka Tandahimba hadi semunge Loliondo.
ReplyDeleteMdau Belgium
anagalieni afya zenu kwanza kila mtu atasema kaoteshwa basi tufunge hoapital hakuna haja ya kua na hosptali tusuburi wanao oteshwa watibu jamani ndoto zimepanda zinashinda upako
ReplyDeleteMichuzi mbona hujatuambia bei ya kikombe,Watanzania tuko juu kwa tiba,sasa hakuna tena kwenda Hospitali.Mungu endelee kutuotesha tufunge Hospitali zote...maskini madaktari wajifunze kulima sasa!
ReplyDeleteWatz mnatia huruma, hivi mnajua thamani ya miili yenu? mbona mnaabuse miili mlipewa na Mungu,? Mi natamani mngejiuliza kabla ya kunywa, halafu bado mnasali au mmesha acha? tutajua vizuri ikifika mwisho wa yote haya maana kila chenye mwanzo kina mwisho na kama wametumwa na Mungu aliyeumba vyote inabidi walokole mjue kwani biblia inasema Mungu hakutuficha lolote, itasikitisha itakapogundulika ametumia mkojo, kinyesi (bora kiwe cha wanyama kuliko cha binadamu)au damu ya wale watoto waliookotwa jalalani ndo mtalia na wakati huo mmeshabugia.Halafu huyu ni mganga.Poleni ila akili zenu zifunguke kwa jina la Yesu.
ReplyDeletewe anony wa kwanza kula tano manake unajua kuzichambua picha.Ni kweli dawa shurti ishushiwe na andazi vinginevyo haifanyi kazi. hapo ni bizness x2. unanunua kikombe na andazi pia..hehehehe bongo tambarareeee.
ReplyDeleteUkiwa umechuka darasa la abnormal pysch watu wengi watakuwa diagnose na Schizophrenia. haluccination na delusional criteria zimewakilishwa toka babu aje na kikombe. Ila darasa linasema tanzania na nchi zingine kuna better outcome za wagonjwa kupona kutokana na support ya jamii. Ikimaanisha ukiwa na pych problem tanzania upelekwi hospital ila unatukuzwa kwamba unafanya miujiza. Inanishangaza muda mwingine lakini ndiyo nchi yangu. mwenyezi mungu tusaidie.
ReplyDelete