Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba le amemkaribisha Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Ofisini kwake Dar es Salaam.  Spika Makinda alifanya ziara hiyo kwa lengo la kupanua mjadala wa maudhui ya kuundwa tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya. Kulia kwa Mufti ni Katibu Mkuu wa Bakwata Alhaji Suleima Lolilya na kushoto kwa Spika ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Mhe. Angela Kairuki. Aidha Spika Makinda pia alikutana na Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania kwa mwaliko wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa lengo la kupokea maoni na ushauri kuhusu uundwaji wa chombo hicho cha kukusanya maoni. Pichani juu   Mufti Mkuu akiendesha Dua maalum kabla ya mjadala kuanza.
 Spika Makinda akiushikuru uongozi mzima wa BAKWATA na kuwaahidi kuwa maoni na ushauri wao vitazingatiwa
 Viongozi wa BAKWATA wkifuatilia mjadala.
 Spika Makinda (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania katika Hotel ya Courtyard, Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekit wa Baraza na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza.
Wajumbe wa Baraza la siasa wakifuatilia mjadala
Picha zote na mdau Prosper Minja wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2011

    Hapa pasisahaulike kuwa sheria ya ubaguzi lazima ianzishwe. Wale waliozoea kubagua watu katika ajira na huduma za serikali wakipate.

    Hatuwezi kuamini tuu viongozi kuwa watasimamia kutokomeza ubaguzi ili hali wao nao waweza kubagua. Iwepo sheria na mwongozo maalum. Hii ni nchi inafuata sheria. Au kufuata sheria kutahatarisha amani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...