Vituo vya TV vya Pakistan vimeonesha picha hii inayodaiwa kuwa ni maiti ya Osama Bin Laden ambayo Marekani imetangaza kumuua leo huko Pakistan. TV hizo zimetoa picha hii inauyochefua kuondoa kile kinachosadikiwa kuwa ni utata kwamba aliyeuwawa sie Osama na hivi sasa uchunguzi wa DNA ya mwili huo unaendelea kuthibitisha kama ni yeye kweli ama boya.

TV hizo za Pakistan zimetangaza pia kwamba wake wawili na watoto sita wa Osama wametiwa mbaroni katika operesheni hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2011

    Hii Picha Ya Uwongo.

    Wewe Ankal ni mpiga picha hivi uoni kuwa Top na Bottom Zimepishana?

    Wameona wamemshindwa sasa wanazushia kifo - POOR FREEMASONS.

    Price Sab

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2011

    Mdau wa kwanza inaonekana wewe ni Al Qaeda pia, na wewe jiandae sasa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2011

    huyo dongo anafikiria nini kumchefua uncle?hajui hata mtoto wake wa karibu wake zake wote wameonyeshwa?huo ni ubishi wa ccm na chadema umemjaa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2011

    duuuu jamani inasikitisha, Mungu amlaze mahali pema peponi na atuepushe na madhara yatakayotokana na kifo hicho

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 02, 2011

    wakati tuliambiwa kwamba Osama hakai na mtoto wala mke kwa miaka kadhaaa tokea tukio la sep 11 sasa mke katoka wapi na watoto hao ki dog ni shaka lakini kumbuka uchaguzi waja wa Usa lazima watoke wanajeshi wa wao watch out

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 02, 2011

    sidhani kama kifo cha huyu mtu kinaleta totauti yeyote kwa marekani kujihami dhidi ya magaidi!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 02, 2011

    wizi mtupu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2011

    INAWEZEKANA NIKWELI KAUAWA...LAKINI HIYO PICHA ILIYOWEKWA HAPO NI FEKI...IMEUNGWAUNGWA WANAITA PHOTOSHOP.JARIBU KUGOOGLE BAADHI YA PICHA ZA OSAMA UTAONA SEHEMU HIYO YA CHINI(HASA MDOMO)KM ILIVYO HAPO.INASEMEKANA PICHA KM HIYO ILIZUNGUKA MTANDAONI MWAKA 2009,WAKATI BUSH ALIVYODAI KAMUUA OSAMA

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 02, 2011

    Mimi naamini kabisa kuwa huyu ndiye Osama muua watu wasio na hatia.
    Nawapongeza wamarekani kwa hatua waliyofikia. Na awayeyeyote mshabiki wa kundi la waovu hawa alaaniwe na ajiweke tayari kufa kifo cha aibu kama cha Osama Bin Laden.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2011

    HATA IKIWA NI KWELI MAITI HITO YA OSAMA LKN INAONESHA NI MAITI ILIKUWA TAYARI IMESHAZIKWA NA HAINA DALILI YOYOTE NI MAITI ILIYOKUWA FRESH INATOKANA NA MAPIGANO.
    NI MAITI INAYOONESHA DHAHIRI KUWA ILIZIKWA NA IMEFUKULIWA TATIZO LA WAMAREKANI HAKUNA WANACHOKIWEZA ZAIDI YA KUWA MABINGWA WA PROPAGANDA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2011

    Poleni kwa wenzetu mnaowafanya wauaji ni "Heroes" wenu. Sasa angalia ameuwawa. Msishindane na jina kubwa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 02, 2011

    Kuna msamiati usemao,kuzaliwa na mwingine kufa, hivyo Osama ametimiza yote, inategemea utakufaje, lakini kufa ni lazima. Sasa cha kushangaa kufa kwa osama ni nini???

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 02, 2011

    KAZIKWA BAHARINI.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 02, 2011

    ndiyo ni Maadili ya Kikristu kutoshangilia Kifo cha Binadamu: Lakini tunakumbuka kuwa huyu ndugu aliua hapo Dar E salaam Ubalozi wa Amerika mwaka 1998: Hivi sasa habari za wahusika wote zipo mikononi wa Pilato hivyo mkae mkao wa kufa, maana mnashuikiwa si muda mrefu: Habri hizi si za campaign--hahhhah --nitaweka Meli ziwa Tnaganyika, ziwa Victoria--- Treni ya Mwendo wa kasi: Hizi ni Habari za Kivita : Mnashukiwa nyote!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 02, 2011

    obama has proved to the world that he's the smartest president ever...i am very happy with the way his men carried out the operation....first of all the operation was very secret to the extent even Pakistan officials and its top intelligent agencies did not know anything not only that but also even those so called allies were not invited...obama knew exactly that some of American allies talk too much so they were put aside...heko obama heko ungeenda nao wangeanza ooh aaa sisi wazu...tumekusaidia kwanza wameshaanza kusema sema mpaka baba wa watu ukatoa birth certificate yako...wapige chini hivyo hivyo tena hasa hawa jamaa waliokuwa na harusi juzi juzi,wangetoa siri buree.BIG UP OBAMA.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 02, 2011

    A fake photo proven.. see video the picture has now withdrawn from all news channels..

    http://www.youtube.com/watch?v=DywpYUgPQMo&feature=player_embedded

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 02, 2011

    Anayeweza kutegua kitendawili hicho ni OSAMA mwenyewe, kama yuko hai atapiga kelele tumsikie! Na wanaosema huyo si Osama wathibitishe! Sadam walisema siye bali ni kanyaboya! Mastermind wa Sept 11 Khalid Sheikh Mohammed walisema si yeye sasa anaozea gerezani!Bado Zawahir! Pesa mbaya! USD 25ml si mchezo! Zinaweza kumnunua na kumuuza kila mtu! Hata Osama!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 02, 2011

    Uncle mdau wa kwanza yuko right, hiyo picha ni fake. Osama amekufa tunajua lakini no matter how graphic that picture is still it is a fake

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 02, 2011

    picha ya uongo.
    angalia hapa http://www.guardian.co.uk/world/2011/may/02/osama-bin-laden-photo-fake

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 02, 2011

    mkuu, acha hizo,
    angalia kwenye facebook, kuna picha kibao kama hizo ,zote zimetiwa u photoshop...mpaka sasa hakuna picha ya osama iliyotolewa popote ,ingetolewa wambea CNN wangekuwa kati ya watu wa mwanzo kusambaza picha hizo.naomba kugoma kuwa hii sio picha halisi kwenye!
    Ysn
    mpanda

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 02, 2011

    kumbukeni, sio mara ya kwanza kusikia Osama amekufa, je mnakumbuka Lile li joji dabwiyuu bushi,lilisema kuwa operesheni ya kummaliza osama ,ilifanyika,na alikuwa amekufa.sasa leo amekufa tena,jamaa anafanana na yesu nini, anakufa na kukufuka?
    waache kutudanganya...mtu kama yule haiwezekani kufa halafu asionyeshwe,au eti kuzikwa baharini,haaiingii akilini.mbona saddam alionyeshwa kitemi kila mtu aone, leo hii ,mtu aliyekuwa akitafutwa miaka mingi auwawe halafu asionyeshwe .hakuna kitu kama hicho.sio kufuata ushabiki tu,walete vyeti kama hawana ukimwi,sio kusema, hawana ukimwi tu nasi tuamini, ndio kusema WATOE PICHA KAMILI na Ushahidi wa DNA hasaa,ili tuamini,sio mambo ya kutulazimisha.
    nawakilisha

    mohsein
    iringa

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 03, 2011

    duh mi tokea mdogo usama amekua ana madevu na mvi saivi miaka 15 tokea nimuone naona yeye anakuwa kijana tu,duh! ina maana hii picha ameshakua kijana tena,halafu anakufa mara ngapi?

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 03, 2011

    Until the U.S. officially states that the photo is authentic do not believe any other photo you see on the Internet, they are all unapproved and fake.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 03, 2011

    Mi hata sielewi yupi wa kumsikiliza. inakuwaje mwili uzikwe baharini bila kuonyeshwa? hii inatia shaka. Mtu alkiyesumbua dunia inakuwaje wamzike/ kumtupa baharini badala ya kumuweka ktk makumbusho ili kila mtu aamini? hiki ni kitendawili jamani?

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 03, 2011

    Poleni sana kumbe madubu wapo wengi hahaha hao wazungu wenyewe wanapiga kelele wamepigwa changa la macho na Mmarekani,huyu Osama picha zake za zamani alikuwa na mvi kwenye ndevu zake sasa mnataka kunambia kuwa kusakwa kote huko alikuwa anapata nafasi ya kutia peacock kwenye ndevu zake ili ziwe nyeusi kama hapo kwenye photo

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 03, 2011

    TANZANIA NDIO TAIFA PEKEE LINALOOMBOLEZA KIFO CHA MTU MWOVU KAMA OSAMA. RAFIKI YANGU SHEMEJI YAKE ALIKATIKA MIGUU KUTOKANA NA OSAMA KULIPUA BOMU UBALOZI. KWA NINI YEYE ASIFURAHI NA KUMSHUKURU MUNGU.

    GOLIATI ALIPOUAWA WANA ISRAELI WALIIMBA NYIMBO ZA MUMSIFU DAUDI NA LUMSHUKURU MUNGU

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 03, 2011

    Osama is either still alive or was killed long time ago by Bush. They were just waiting for the right time to release the news for political gain.

    Kwa Kiswahili: Osama hajauwawa juzi. Aidha yu hai au alishauwawa siku nyingi na Bush, ila Obama ameamua kufanya usanii ili apate umaarufu wa kisiasa.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 03, 2011

    kwa imani za dini haitakiwi kuoneshwa mwili wa marehemu au nakosea? nisaidie bwn mohsein wa iringa, manake msitafte maneno mengine zaidi ya ugaidi yakaja malumbano ya kidini baadae watu hawaheshimu imani za watu, kama yupo basi atokee lakini sio mwili wa mtu aliyekuwa na imani yake kutolewa hadharani, pia kuuweka mwili sana nayo hairuhusiwi naonaga wenye imani hii hawaulazi mwili labda kuwe na sababu maalumu....kuhusu sadam hussein sikumbuki kuona maiti yake zaidi process za mauwaji tena kwa wale waliofanikiwa kuiba pics kwa kutumia camera basi.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 03, 2011

    TEHE TEHE OSAMA,OBAMA,OSAMA,OBAMA, EBU ANGALIENI JINSI MAJINA YAO YANAVYOFANANA KASORO HERUFI MOJA TU HAWA WATU WAWILI NI BABA MMOJA KASORO MAMA TU,BABA YAO ALIAMUA KUWAPA MAJINA YANAYOFANANA ILI WASIJE KUPOTEANA.
    TEHE TEHE KAZI IPO MAITI HIYO INAONEKANA IMESHAOZA YASIKUNYINGI SIO KAMA WANAVYOSEMA IMEUWAWA ALFAJIRI ASUBUHI IWE IMESHAOZA JAMANI HEBU KUNENI VICHWA NA MUACHE USHABIKI.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 03, 2011

    Huyo sio Osama jamani! acheni kutuchanganya nyie Wamerekani, kama yamewashindwa si mseme tu mmeshindwa? Osama yuko Haiiiiiiii.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 03, 2011

    Video yake ya 2004 anamuonyesha Osama akiwa na mvi nyeupe, sasa hivi ni miaka 6 imepita tokea atoe video tape yake ya mwisho. sasa inakuwaje mvi badala ya kuongezeka zimepungua??? Uongo mtupu labda wamemuuwa OSAMA LOOKALIKE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...