kwanza kabisa nashukuru sana na ninakupongeza sana kwa juhudi zako binafsi za kila siku na kutujuza Dunia inakwendaje kwa ujumla. mimi ninashida moja ninaomba Maoni au msaada,


mimi ni Mwanaume wa miaka 28, nina msichana wa miaka 25 tunapendana sana, hususan yeye ananipenda sana, yani to the maximam point kiasi kwamba muda wote huwa anataka kuwa na mimi mpaka muda mwingine nachoka, yani mpaka nikimwambia naenda kucheza mpira huwa hapendi anataka tu niwe na yeye muda wote. bila shaka na mimi ninampenda sana, na kutokana na ndoto zangu ni aina ya Mwanamke ambaye nataka awe mke wangu ndani ya mwaka 1 au 2 ijayo.

Ila kitu ambacho mimi sivutiwi kwake ni kwamba 'Nyumbani Kwa Mfalme Suleiman' kuna pafyumu kali ambayo mimi siipendi hata kidogo, hata kama akitoka kuoga muda huohuo na kutumia sabuni za kike za kusafishia hiyo nyumba pafyumu huwa bado ipo, mpaka mara kwa mara hisia zinakuwa zinanitoka, hali hii inasababisha au inanipelekea mimi kumkumbuka sana Girlfriend wangu wa zamani na kujikuta naumia moyo sijui la kufanya. sababu yule wa zamani alikuwa hata akae siku 2 bila kuoga sikuwahi kusikia pafyumu. basi nilikuwa naenjoy nae sana lakini tatizo lake alikuwa ni mkorofi sana kila siku Ugomvi ikapelekea kuachana.



Nipo katika dilema naombeni wana blog mnipe ushauri au nifanye nini ili kumsaidia huyu msichana wa sasa ambaye anasifa zote za kuwa mke ila tatizo ni hilo tu la pafyumu. but she is very beautifu yani anafigure namba 8, yani nakuwa confortable zaidi kutembea nae barabarani kuliko kula nae chakula cha usiku. tangu tumeanza mlo wa usiku sasa hivi tuna miezi 6. na sijawahi kumwambia hata siku 1 kuhusu hilo tatizo kwani naogopa kumdiscourage na kumfanya ajisikie vibaya huwa tu namsifia muda wote. kitu kinachonipa confidence ya kuendelea kuwa nae ni kwamba kipindi ambacho sijaanza kula nae chakula ya usiku nilikuwa nasikia vijana wa kiume wakisema Kwa Mfalme Suleiman kama hautoi pafyumu basi ni shetani au jini. hiyo ndio inanipa confidence. lakini msichana wangu wa kwanza alikuwa hana pafyumu, na katika maisha yangu huyu ni msichana wangu wa 2. wa kwanza nilikaa nae miaka 3. je nifanyeje?



please please, am seriously seeking 4 help

Mdau Pwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2011

    Mtafute Gynaecologist (kama upo Dar watakuwepo muhimbili, au hospitali yeyote kubwa). Ongea na Daktari kuhusu tiba yake, kisha mueleze mwenzio kiupole na kwamba umemtafuta mtaalamu tayari.

    Ukimpeleka Samunge, kwishnehi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2011

    Dogo hiyo issue ndogo sana...........mwambie atumie dettlor inaclear harufu yote........

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2011

    Pole kaka,
    Mimi ni msichana naelewa mambo hayo. Labda Ana some sort ya infection Kama bacteria viginosis ..ni muhimu kwenda hospital kucheki , mwambie tu politely ..mwende wote ili mtibiwie wote.. Maana vitu lvingine haviaffect male lakini unaweza kumpa tena baada ya yeye kupatA matibabu.

    ReplyDelete
  4. Anaweza akawa ana ugonjwa, aende hospital kuona wataalamu.........

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2011

    Mzee wa libeneke kwanza nakupongeza kwa kuruhusu demokrasia ichukue mkondo wake humu blogini mwako, japo naamini na nitakuwa sikosei nikikuomba usiruhusu tena haya makala ya aina hii humu ndani, kwani hii ni blog ambayo ina heshima yake. Lakini pamoja na kusema haya yote naomba nimshauri huyu mdogo wangu kama ifuatavyo:

    Kuoa au kuishi na mwanamke kama mume na mke ni majumuisho ya mambo mengi mdogo wangu na si kufanya ngono tu, japo sawa na hilo ni issue ya kuzingatia. kwa hali hiyo kama kweli unampenda naamini utamlinda. utamlinda vipi basi ni kwa kukaa na kuongea nae juu ya hilo. Hakuna jambo lisilo na suluhisho chini ya jua, lazima kuna namna mtapata usuluhishi. kama ulivyotudokeza, wewe bado ni mchanga sana katika ulimwengu wa mapenzi na nafikiri hata huyo mwenzi wako yu vivyo hivyo, kwa hiyo ni mapema mno kuchukua maamuzi mengine zaidi ya kutafuta suluhisho.
    kwa jinsi nilivyofuatilia mazungumzo yako, suala lililopo ni kwamba wewe unapenda sana ngono na inaelekea huyo mwenzi wako kakua kimjinimjini (hakufundwa) na kufundishwa jinsi ya kusafisha nyeti zake, kwa hali hiyo kwa kuwa mara kwa mara unapenda kufanya naye tena bila condom its most likely anashindwa kumaliza mawaa yako ndani ya utupu wake pale anapoosha baada ya kujamiiana, anyway hayo ni kwa mtazamo wangu.
    Lakini kama nilivyosema ni vyema mkaongea, umueleze ukweli halafu mfike muafaka, kama ni kuwaona wakubwa au madaktari lazima mtapata suluhisho. Mwisho napenda nikukumbushe kuwa "SI KILA KING'AACHO NI DHAHABU'

    AHSANTE!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2011

    Pole sana Bw. mdogo, lakini ushauri wangu ni kwamba unachotakiwa kufanya ni kumsaidia. Kumsaidia kwenyewe ni kumwona Daktari kwasababu mara nyingine sisi wanawake tunakuwa na magonjwa ambayo sisi wenyewe hatujijui kwa sababu hakuna maumivu unayoyasikia huko kwa Mfalme Suleiman tunajihisi ni wazima na hasa harufu ikitoka kwako mwenyewe huisikii.

    Kivumbi kinakuja ni jinsi gani utaweza kumweleza. Kwa kweli hata na mimi ni mwanamke lakini kuambiwa kitu kama hicho na mpenzi wangu sitajisikia vizuri. Nakushauri ongea na Daktari kwanza mweleze hali halisi alafu wewe ndio ujifanye mgonjwa huko kwa babu na ili kujua kama umemwambukiza au la akapimwe na yeye hapo ataonekana kama anafangasi au la inategemea Daktari atasema nini, maana hata fangas wanasababisha harufu hasa wakiwa kwa ndani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 17, 2011

    Kaka pole kwa yakupatayo.
    Nimeipenda nia yako njema ya kuomba msaada. Hii itakusaidia wewe na watu wengine wenye tatizo kama lako maana haiyumkini wako wengi humu ambao hawajapata udhubutu wa kuomba msaada.
    Kwanza kabisa hali ya mwenzio inaweza kuwa imesababishwa na ugonjwa uitwao Bacterial Vaginosis. Huu ni ugonjwa usababishwao na bacteria ambao hukua kwa wingi ukeni. Mara nyingi hutoa harufu kali kama ya samaki aliyeoza au zaidi ya hapo.
    iwapo harufu hii inafanana na mkate uliooza, itakuwa ni maambukizo ya fangasi. Hali zote hizi hutibiwa hospitali na kupona na harufu hutoweka.

    Ni dhana potofu kuwa ni lazima mwanamke atoe harufu mbaya ukeni. Mwanamke alie msafi vya kutosha na asiye na maambukizo au magonjwa mengine sehemu za siri, hatoi harufu. Hata hivyo wapo wengine wenye harufu kidogo kwa asili yao lakini si harufu inayokera.
    nakushauri umpeleke mwenzio kwa daktari wa kina mama au waweza wasiliana nami kwa barua pepe saprima@gmail.com
    Dr. Primus

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 17, 2011

    kuna watu humu ndani, napenda sana wanavyochangia mada, hili jambo liko soo sensitive hata kulielezea kwake,ni kweli kuna vigonjwa vidogo, vidogo vingi vya kibinaadamu ambavyo unaweza kujiona umzima, kumbe ni mgonjwa, hivyo ndugu yangu nenda kamuone daktari mueleze halafu fuata ushauri na uanze kuufanyia kazi, then uoe ule halali meat yako!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 17, 2011

    Hiyo itakuwa ni STD au magonjwa ya ngono, dawa yake ni anti-biotic lakini iwe ni maalum kwa ajili ya kutibu hao bacteria waliomo kama alivyosema mdau hapo juu ni bacterial vaginosis dawa yake ni kupata dozi moja ya 2g ya flagyl inatibu haraka.. hiyo harufu huambatana na muwasho kuna dawa inaitwa canesten duo huwa inasaidia.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 17, 2011

    dawa inaitwa Flagyl ama Metronidazole

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 17, 2011

    Pole sana Broo.... nimependa ulivyotumia lugha ambayo haichafui hali ya hewa. 'PAFYUMU NYUMBANI KWA MFALME' mi nilijua hadithi ila baada ya kusoma nimeelewa. Ushari mweleze hali halisi ki-saikolojia then mwongozane kwa docter kwa matibabu zaidi.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 17, 2011

    pole sana mkuu

    Mwili wa binadamu umeumbwa na una components ambazo ni very nutritious kwa vijidudu kama bacteria, Ni bacteria hao wanaosababisha harufu mbaya sehemu mbalimbali za mwili ijapokua mwili kama mwili hauna harufu mbaya, cha kufanya wewe km mzazi mtarajiwa ongea ki utu uzima na mwenzio mkamuone mtaalamu kama watangulizi walivyomuita Gyanacologist na mambo hayo yataisha.

    Kuhusu detol, mimi ni mtaalamuwa Biotechnology na maabara kwa ufinyu wangu wa mawazo sikushauri utumie detol kabla ya kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu kwa kua sabuni hii inauwezo mkubwa sana wa kuuwa bacteria wengi wakiwamo wale ambao wanafaida kwa sehemu husika ambao vilevile wakitoweka inaweza kuleta matatizo kwa eneo husika kuvamiwana bacteria wengine,

    Ahsante sana,

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 17, 2011

    Mwache,tafuta mwingine!! wapo wasiokuwa na pafyumu au hujui kwa kuwa huyo niwa pili!

    ushauri wangu changanya na wa kwako! mbayuwayu!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 17, 2011

    mwache huyo hajui usafi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 17, 2011

    Ndugu yangu Michuzi. Nakushukuru kwa kutuunganisha watanzania wa ndani na nje kwa njia ya blog yako maarufu. Pengine ungefungua blog nyingine ambamo watu wangejadili maswala sensitive kama hili la ndugu yetu. Mwanangu anaitumia blog yako kujifunza kiswahili, na nimepata taabu kumfafanulia yale uliyoandika kwa sababu ya aibu zetu watanzania kama unavyojua. Nakuomba kwa heshima yote, mijadala ya aibu iwekwe kwenye blog nyingine ili blog yako mahili izidi kusonga mbele. Mungu akubariki

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 17, 2011

    Hebu nipe namba yake ya simu au e-mail adress yake nikusaidie kurekebisha hiyo hali bila wewe kupata kigugumizi wala kujua, utaona tu hali imebadilika.


    Kiberiti Upele, Columbus Ohio

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 17, 2011

    Mficha uchi, hazai. Kauli hii ya wahenga wetu ikufikie wewe Anonymous wa 09:2100 unayemtaka Ankal afungue blog ingine watu wajadili masuala ambayo wewe unayaita sensitive na ya aibu. Mie sikubaliani nawe kabisa kwani kwa taarifa yako blogu ya jamii imekuwa nambari wani kutokana na mijadala ya namna hii, kwa lugha ya kistaarabu kiasi kwamba hata hali ya hewa haina pafyumu. We unadhani kufungua blog mchezo sio? Wangapi wamefungua (na Ankal anajitolea kuwatangaza bila kinyongo) lakini leo wako wapi????? Nyie ndio mnaomuonea gere Ankal kwa kuwapiga bao kiasi hata watangazaji wanashikana mashati kutaka kuonekana humu kwa jinsi utitiri wa watu unavyomwaika humu kila saa. Acha wivu na ukuda wako, kama u mvibu kuwafundisha watoto wako that is ur problem sir/madame! Acha sie tupate kuondoa stress zetu za maboxi huku tukipata somo la mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mada kama hizi ambazo kama alivyosema mtoa mada, ni chachu ya blogu ya jamii ambayo haina mfano. Acha hizo kabisa mjomba/shangazi. wewe kama vipi mkataze mwanao asifungue. Kama lugha ingetumika sivyo ndivyo hata mie ningekuunga mkono. Ama unataka kutuambia kwamba sex education hapati mwanao shuleni kwao ama sehemu ingine. Aibu unaijua wewe.....Alaaaaaaahhh hebu tuondokee huko

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 17, 2011

    acheni kutoa ushauri usio jenga.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 18, 2011

    hebu mwambie huyo mpenzi wako asisafishe nyumba ya mfalme na sabuni yoyote atumie majituuu.
    unajua hua tunadhani usafi nikutumia sabuni nononoononon
    Nyumba ya mfalme hua ina bacteria ambao wanailinda isipate maambukizi sasa ukianza kuiosha na sabuni unawaua hao bakteria tena aliye sema Deto nampinga vikali na matokeo yake unapata maambukizi then harufu .
    aoshetu vizuri na maji.
    mimi ni binti hua naosha nyumba yangu na majitu na BF wangu aliwahi niambia kua kati ya wanawake wote amewahi kuwa nao ni mimi peke yangu nyumba yangu haina harufu.
    pia mambo yakujiingizia vidole wakati wakuiosha kwamadai ya kujiswafi eti ndio kufundwa wataalam wanasema haitakiwi just osha na maji lile eneo basi huko dhani kutajisafisha na vitu vitatoka vyenyewe kwawakati wake then utaosha

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 18, 2011

    Wewe una busara sana tumia lugha hii hii uliyotumia kwenye hii story yako kumueleza mwenzako hisia zako halafu mjadiliane namna ya kutatua na mwishoni mapenzi yenu yatadumu zaidi badala ya kuharibika. Eti "Nyumbani kwa mfalme Suleiman..." ha, ha , haa! Umetoa wapi hii?

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 18, 2011

    Wakati tukiwa wachumba mke wangu alikuwa na tatizo hilo, nilimwambia atafute jinsi liishe, sijui alifanyaje, baada ya muda likaisha na tukaoana, hadi sasa halijawahi kutokea na tuna miaka sita katika ndoa, tatizo hili pia linasababisha pango kuwa na ukame kama wa jangwa na mtu akilazimisha sana anaweza kujeruhiwa gongo lake la kifalme. Tatizo hili si uchafu ila nafikiri ni infection kama waliotangulia walivyosema. Nasikia harufu hiyo pia inachangiwa na dawa za kupunguza ulegevu wa pango la mfalme.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 18, 2011

    Unajua watu wanapenda kujidai wastaarabu, eti Blogu inaheshima, eti mi aibu, ndugu zangu nimegundua habari nyingi amabazo mnadai ni za heshima hamzichangii kama hii (michango zaidi ya 25). Hapo utaona kuwa nyinyi wenyewe mnapenda. huyo aliyeomba ushauri ameomba kwa watu amabao anajua ni wakubwa na wastaarabu ili apate ushauari kwa usahihi, pia ametumia lugha safi sana ambayo ni tafsida tosha, naomba tukumbuke kuwa yeye hakupenda kuomba kwa blogu za kidaku ili apate ushauri wa maana.
    USHAURI.
    Ndugu yangu kama upo Dar nakushauri uende muhimbili ili upate tiba sahihi, kwani ni Daktari pekee atakayeweza kuongea na mpenzi wako ili amuelewe, vinginevyo utamkosa mpenzio.

    Ahasante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...