Umati wa abiria ukisubiri huduma kituo cha Ubungo leo
Kina Ras Makunja wakitawanya makonda na madereva waliotaka kuleta rabsha baada ya kugoma
Madereva wa mabasi ya abiria yanayokwenda mikoani na nchi jirani leo asubuhi waliamua kusheherehekea Sikukukuu ya Mei Mosi kwa staili ya kugoma kushinikiza maslahi na namna bora ya kufanya kazi.
Kitendo hicho kimefanya maelfu ya abiria wanaokwenda Bara majira ya asubuhi kutoka Kituo kikuu cha Mabasi cha Ubungo kuchelewa kuondoka kutokana na mgomo huo.
Imeelezwa kuwa mgomo huo ulikuwa na lengo la kushinikiza mambo mbalimbali ambayo hayajapatiwa ufumbuzi kwa miaka minne sasa, likiwamo suala la ajira.
Mgomo huo uliisha saa 6.40 baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu. Mbali na suala la mikataba ya ajira madereva hao wanataka fedha iliyotakata ya sh 350,000 kwa mwezi kama mshahara na kuwapo kwa posho ya safari na polisi kuacha kuwaonea.
Kama itakumbukwa mwaka jana waligoma kwa sababu hizo hizo.
Kina Ras Makunja ambao ni maarufu kwa kutulkiza boli waliitwa
kuweka displini kama unavyoona.


Jamani kwa nini wamiliki wa mabasi wasiwape hiyo 350.000,tena kulingana na hali ya maisha ya sasa haitoshi kabisa!
ReplyDeletePolisi wataendelea kuwaonea,kuna msemo mmoja madereva wanasema kwamba polisi wakikukamata lazima watakuona una kosa kwa hiyo basi hata ukitoa gari dukani leo Polisi akikukamata atakukuta una kosa RUSHWA
ReplyDeleteHuu ni umoja ambao kwa sisi ni vigumu kuweza kuendesha mgomo maana kuna madreva wengi ukigoma watapewa gari hapo hapo,tajiri anatafuta dreva hata kama ana leseni,ili mradi apate pesa kwa siku hiyo.
Sisi watanzania kuna udhaifu mmoja tunao wa kumdharau mtu hata kwenye mablog humu hiyo tabia hipo kwa hiyo hilo ni JANGA LA KITAIFA kumdharau mtu pasipo kujua wewe unayemdharau una leta madhara gani kwa taifa kama watu watasema HAO MADREVA HATA SHULE HAWAJAENDA WANAGOMA NINI AU UPO KWENYE BASI UNA SAFIRI DREVA AKIMINYA BREKI GHAFLA BILA KUJUA KITU GANI ABIRIA WANAANZA KUMTUKANA DREVA MPAKA DREVA ANAGOMA KUENDESHA GARI,MNAANZA KUMPEMBELEZA DREVA.
Lakini abiria hawamueshimu kwa kutokujua dreva ni muhimu ameshikilia roho zao.TUNA SAFARI NDEFU NAWAKILISHA HOJA
Mimi nafikiri pia hata madreva wanamakosa.Kwa sababu hakienda kuomba kazi kwa mwenye basi wanongea nini na wanakubaliana nini?Maana mimi najua ukiomba kazi utaitwa kwenye usaili baadae utaulizwa unataka nini na mshahara kiasi gani then unapewa mkataba wa kazi.Sasa wao wanataka mkataba upi?Maana hayi mikataba walitakiwa kupewa kabla ya kuendesha hayo mabasi. Pia wajue hayo mabasi ni ya kampuni tofauti ambazo zina sera tofauti.
ReplyDeleteMZEE WA IFAKARA