Timu ya mabingwa wa Mwendelezo wa Msimu Dhahabu unaoendelea na Serengeti Soka Bonanza Mkoani Tanga mashabiki wa Manchester United wakiinua juu kombe lao, mara baada ya kushinda katika mchezo uliowakutanisha dhidi ya wapinzani wao wa kweli timu ya mashabiki wa Barcelona mkoani humo na Barcelona kufungwa kwa penati tatu kwa moja baada ya kutoka suluhu katika dakika za kwaida kwenye bonanza lililofanyika leo kwenye uwanja wa Mkwakwani  jijini Tanga.
Mashabiki wa Man U wakiwa wamemnyanyua mmoja wa wachezaji wao mara baada ya kufunga mkwaju wa penati na kuwa ndio mwisho wa mashabiki wa timu ya Barcelona. Mchezo huo umefanyika leo kwenye bonanza la Serengeti Fiesta Soka, uwanja wa Mkwakwani  jijini Tanga. Baada ya Man U kupigwa 3-1 na Barcelona wa ukweli jana hii ni kama kafaraja ka jamaa zetu hawa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2011

    Ovyooooooo,hamna majina ya kujipa mpaka ya wenzenu,mmeomba copyright za hizo timu au?tunajidharau wenyewe bila sababu, sasa tuseme ukoloni mambo leo au utumwa wa mawazo.Umeona simba au Yanga Uingereza au Spain....Ovyoooo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2011

    Ankal huyo jamaa aliyebebwa anaonekana hewani ndio Guadiola wao?au ni macho yangu? Ahhh kumbe ni mkwakwani,mi nilidhani ni Wimbley, maana mpaka malkia alikuwa anaishangilia Barca jana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2011

    Habari nyepesi nyepesi na za kuaminika: Ferguson mwenyewe jana alikuwa anashabikia barca baada ya kuona ngoma nzito, pale walipogombana na Rooney maelezo yalikuwa kama yafuatavyo:

    Rooney: Mzee mbona umetugeuka?
    Ferguson: Wee fwala nini?, wenzenu wanacheza soka nyie mnacheza kiduku? rudi uwanjani mkaongezwe mkong'oto
    Rooney: Sasa ina maana unashabikia Barca?
    Ferguson: kamuulize Messi! nyambaaf! mkubwa, Huyo malkia mwenyewe leo yuko Barca itakuwa mimi?
    Rooney: Lakini mzee, mbona na wewe nimekuona uki vibrate baada ya kuona zile pasi za Barca?
    Ferguson: Kudadeki, rudi ndani hujamwona mwenzako Fabio kapigwa chenga hadi nyonga zimestuka.
    Ferguson: Ukirudia tena msimu ujao nakuuza Blackpool au utasaga makalio benchi! Kichwa kama dafu la Jamaika.
    Rooney: Samahani mzee, Pamoko sana, aminia mazee !

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2011

    Naungana na mchangiaji wa kwanza hapo juu,kwanini hizo timu za mikoani kwetu zisitumie majina ya timu zetu za TZ km simba,yanga,pan africa,kagera star,pamba na nyingine nyingi tu,hata wadhamimni nao naona bado wana utumwa wa mawazo na akili.Jamani tujiamini km watanzania na tutaweza na tutahemiwa pia lkn km tunashindwa kutangaza timu zetu mnafikiri hao man u na barc ndo watatutangazia?tuamke usingizini especially WADHAMINI WAKUU WA HAYO MATAMASHA LOL!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...