Nahodha wa timu ya soka ya wanaume ya Umisseta kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero,Hussein Njechele , akipokea kombe la Ubingwa wa Mkoa wa Morogoro wa mashindano ya Umisseta ngazi ya Mkoa kutoka kwa Ofisa Elimu wa Mkoa huo, Fatma Kilimia , ambaye ni Mwenyekiti wa Umisseta Mkoa .Kilombero walitwaa taji hilo baada ya kuifunga Manispaa ya Morogoro mabao 6-4 ya mikwaji ya penati baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90.Nahodha wa timu ya soka ya wanawaake ya Umisseta kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Ziada Ramadhani, akipokea kombe la Ubingwa wa Mkoa wa Morogoro la mashindano ya Umisseta ngazi ya Mkoa kutoka kwa Ofisa Elimu wa Mkoa huo, Fatma Kilimia , ambaye ni Mwenyekiti wa Umisseta Mkoa . Kilombero ilitwaa taji hilo baada ya kuifunga timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa mabao 21-19.
Mchezaji wa kuruka kamba wa timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ya Umisseta, Maua Omari , akiruka kamba na kufanikiwa kushinda na kuchaguliwa katika timu ya Mkoa wa Morogoro ya Umisseta.
Baadhi ya Wachezaji waliochanguliwa kuunda timu ya soka ya wanawake ya Umisseta ya Mkoa wa Morogoro kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ,wakijawa na furaha kwa mkumbatia mwalimu wao aliyetambuliwa kwa jina moja la Mchuma ( kulia) baada ya kamati ya michezo ya michezo ya Mkoa kumchangua kuwa mlezi wa timu ya Mkoa ya Umisseta.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...