
Msanii wa kikundi cha KAKAU anayedaiwa kuwa kiwembe akishangilia matokeo ya vipimo vya afya ya mke wake aliyeko kulia kabisa, fataki huyo aliyemkumbatia ni mmoja wa mahawala zake, fataki huyo alikuwa akishangilia kwa madai kuwa kwa kuwa mke wake amekutwa ajaathirika na hiyo na yeye hajaathirika, fataki huyo alikataa kupima afya yake.

Muigizaji wa kikundi cha KAKAU kinachomilikiwa na kanisa Katoliki la Bukoba akilia kwa uchungu baada ya mume wake kukataa kuambatana naye kwenda hospitali kupima afya zao, Msanii huyo alidai kuwa ana mimba na mme wake ambaye pia ni muigizaji ni kiwembe hapitwi.

Inawaonyesha wasanii wa kikundi cha Burasinga kilichokuwa kinachuana na vikundi vingine vya sanaa ambavyo vitashirikiana na na mfuko wa mama Salma Kikwete (WAMA) unaofanya kazi ya kuhamasisha wanawake wapime virusi vya ukimwi wanapopata mimba ili waweze kukabiliana na maambukizi ya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto. Picha zote na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii,Bukoba


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...