Naibu Waziri wa TAMISEMI,Mh. Kassim Majaliwa, akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Michuano ya Kill Taifa Cap mwaka 2011, Kaptani wa timu ya mkoa wa Mbeya, Ivo Mapunda baada ya timu ya mkoa huo kuibuka washindi baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Mwanza goli 1-0 wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Wachezaji na viongozi wa timu ya Mkoa wa Mbeya wakiwa na Kombe la Ubingwa
Wachezaji wakiwa na Kikombe na mfano wa hundi wa Sh Milion 40 walizokabidhiwa baada ya kukabidhiwa

Na Mwandishi Wetu,Arusha.

TIMU ya Mkoa wa Mbeya (Mapinduzi Stars) imenyakuwa ubingwa wa michuano ya Kili Taifa Cup baada ya kuifunga Mwanza goli 1-0 katika mchezo wa hatua ya Fainali uliyofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mjini hapa leo.

Dakika ya 88 ya mchezo,Mshambuliaji wa timu ya Mkoa wa Mbeya,Gaudence Mwaikimba aliwanyayua mashabiki wa soka na wapenzi wa Mbeya baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi iliyochongwa na mchezaji mwenzie,Mwagane Yeya na kujaa wavuni.

Mbeya imejinyakulia kitita cha sh.milioni 40, huku washindi wa Pili timu ya Mwanza wakiondoka na sh.milioni 20 na mshindi wa tatu Ilala ikiibuka na sh.milioni 10.

Katika mashindano ya timu, Timu ya Ilala imeibuka na zawadi ya timu bora yenye nidhamu na sh.milioni 2.5, wakati mchezaji Bora ni Juma Mpola wa Mbeya ambaye amepata kitita cha sh.milioni 2.5, mfungaji bora ni Gaudence Mwaikimba alimejinyakuwa kitita cha sh.milioni 2 baada ya kufunga magoli 8.

Mwamuzi Bora ni Israel Nkongo aliyepata kitita cha sh.milioni 2, kipa bora ni Abdul Juma wa timu ya Ilala aliyejinyakulia kitita cha sh.milioni 2 na Kocha Bora ni Juma Mwambusi wa timu ya Mkoa wa Mbeya ambaye nae amejipatia kitita cha Sh.milioni 2.

Mgeni rasmi aliyekabidhi zawadi hizo alikuwa ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI,Kassim Majaliwa.

Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager na masuala ya habari kuratibiwa na Kampuni ya Executive Solutions.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2011

    Huyu Mwaikimba vipi huyu. Kwenye makombe ya mbuzi anatesa kinoma lakini anashindwa kuchegama na mabeki wa kimataifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...