Mbunge wa Viti Maalumu Vijana CCM) Mh. Catherine Magige, leo ametembelea kijiji cha Maji ya Chai Wilayani Arumeru na kumsaidia mwanamke mwenye uzazi wa ajabu, Bi Chausiku Suleimab, ambaye anabeba mimba kwa miaka mitatu na hivi sasa ana watoto 18. Vile vile ana mimba nyingine iliyodumu miaka 3.
Mh. Magige amempatia msaada Mama huyo kwenda Loliondo kwa Babu, amemlipia kodi ya nyumba kwa mwaka mmoja, pamoja na kuta ada ya shule kwa watoto wake watano.
Mh. Magige pia alitembelea Magereza na kuongea na wafungwa ambako alijitolea kuwalipia wafungwa zaidi ya 10 fedha za faini ili waachiwe huru. Wafungwa wamemshukuru sana Mbunge huyu kijana kwa kuwatembelea.

Bi Chausiku Sulemani Mkazi wa Maji ya Chai wilayani Arumeru anayezaa bila kupumzika na kila akizaa anaacha mtoto mwingine tumboni baada ya ujauzito wa miaka mitatu

Bi Chausiku akilia kwa uchungu wakati akielezea mateso yake ya zaidi ya miaka 15 ya kuzaa bila kupumzika huku akiwa hajakutana na mume wake kimwili
Mbunge wa Viti maalumu Mh. Catherine Magige akimpatia
Hili mbona suala ambalo serikali inatakiwa kuliingilia kati. Inamaana anajifertilize mwenyewe bila mume?
ReplyDeleteuchunguzi ufanyike baba wa hao watoto ni nani? sio kusikiliza simulizi na kuishia kusikitika. Maana pia bongo kuna mawili:
ReplyDelete1. stori kama za mtu nyoka
2. watu kugomea nyota ya kijani
SAMAHANINI WAUNGWANA SIJAELEWA UZAZI WA HUYU MAMA KWANI KUULIZA SI UJINGA,HABARI INASEMA ANAPATA UJAUZITO BILA KUKUTANA NA MUMEWE KIMWILI KWA MAANA YA KWAMBA ANA MUME,SWALI LANGU NI KWAMBA INAWEZEKANA JE?NINGEPENDA KUFAHAMU KWANI MIMI NI MCHUMI NA MAMBO YA UDAKTARI NA UZAZI NINAYO FAHAMU NI MACHACHE SANA-by DAKO.
ReplyDeleteWadau habari kdg haipo wazi sana hasa ktk idadi ya watoto alonao,muda wa kubeba ujauzito na namna anavyopata ujauzito bila kukutana na mumewe.Yani kuna mswali mengi yanayohitaji majibu hasa ktk scientific point of view.Anyway,vyovyote itakavyokua kitu kimoja kipo wazi ambacho ni kwamba huyu mama hazai ktk hali ya kawaida.hivyo basi kwa nini asipelekwe hospitali akatolewe Overy na au Uterus na watu waamue kumpeleka kwa babu km mnavyomuita.Me naona operation ingekua solution ya uhakika zaidi kuliko huyo babu yenu.Tena huyu alojitolea ni mbunge au alishampeleka hospitali ikashindikana.Tuwe wenye kufikiria japo kdg hata km ndo tumekuwa mbumbumbu kiasi hicho.Kule kwetu twasema KUONA KUONO MAKELE PIA KUNA?
ReplyDeleteMdau AbuObaidah At-Tanzany.
Mhhh!maana sijui nianze wapi niishie wapi.Kwanza labda nimpe pole mzazi kwa matukio hayo yanayomkuta lakini ni alama ya kuuliza ktk kichwa changu hapa nilipo.Na pili ninampa pongezi kwa mbunge huyu kwa kujituma na kujua hali ya maisha magumu kwa mzazi huyu pamoja na kuchukua jukumu la kuwalipia ada watoto watano.Ila mbunge kidogo nadhani kama atakuwa amekosea jambo moja kwa mimi nionavyo.Kuliko kumpeleka kwa babu nadhani ingekuwa jambo muhimu kama angemsaidia kumuombea serikalini wampatie matibabu kwa madaktari wahusika na wazichunguze hizo mimba zinatokea wapi na DNA kwa watoto zichukuliwe ijulikane kama wanachangia baba mmoja au ni vipi.Kwa "babu"anatoa kikombe tu na ni "abdakadabra"tu hakuna kitakachomsaidia hapo.Hao watoto wanatia huruma ikiwa kama watakosa malezi bora kutokana na kuwa wengi na huduma ni chache.Yaani huyu mama kwa nchi za wenzetu ingekuwa ni ishu kubwa na serikali ingegharamia kumpeleka kwa mabingwa wa madaktari ili wajue kinachoendelea.
ReplyDeletekuto elimika, kutojua mtoto anakaa tumboni miezi mingapi. watu wa kijijini usema mtoto ukaa tumboni miezi 12, huyu mama kazidisha sasa anasema miaka 3, duh!!! Au akili zake sio nzuri? hata huyo mbunge kasoma shule gani jamani? Hata mtoto wangu wa miaka 14 anajua mimba inakaa tumboni miezi 9, na sio miaka 3. Badala ya kupeleka uzazi wa mpango vijijini munampa ela aende kwa babu aise,, huko kwa babu akatoe mimba?
ReplyDeletemie nazani huyu mama anazaa kama inavotakiwa, au tuseme akili zake sio mzuri au hajui. anabeba na kuzaa tu basi. Na hajui kuwa siku moja tu mimba inaingia, maana wengine wanafikiri wafanye mwenzi mzima kila siku ili mimba ingie, kutosoam
ReplyDeleteHadithi imeandikwa kimkato sana kwa hiyo maswali niliyonayo sijui hata nani wa kujibu
ReplyDelete2. Babu siku hizi ameongeza magonjwa ya kutibu? Si tuliambiwa ni magonjwa sugu tu yanayowasibu watanzania. Common people....Hii inatia aibu...kama ni kweli yanayomsibu huyo mama apelekwe kwa dr na waangilia dna hao watoto. Ina maana toka alipozaa mtoto wa kwanza wengine wanaengezeka tumboni tu kama tegu? Na kama kila mtoto anachukua mimba kwa miaka 3 hivi sasa angetakiwa kuwa ajuza ...yaani tuassume alianza kuzaa na miaka 12 plus 54 angekua 66...menopause haimkuti yeye na mbona haonekani mzee...Hebu mtwandikie vizuri sio mkato mkato...
Huyo anahitaji dr na sio babu. Afundishwe uzazi wa majira na pia wamcheck akili yake. Anaweza halali na mumewe lakini analala na watu wengine bila kufahamu. Mume anaweza kusema mimi sijafanya kitu naye lakini hujui anapata wapi hao watoto. Huwezi sema yai linakua fertilized lenyewe. Hii tunahitaji kisomo sana kwa vile bongo hatufundishani haya mambo kabisa ni kungoja upelekwe kumtembelea bibi na siku hizi bibi wenyewe wa mjini hata hawajui kueleza kitu. Mimi nilikua mpaka form three sijui the process of baby making na ile kuacha darasa la biology ndio hivyo sikujua chochote. Hatujui the ovulation process na why girls have menstrual cycle yote hayo hatujui nfio maana matokeo yake ndio hayo...kwa babu....
ReplyDeleteHuwezi zaa bila mwanaume...hata kuku wa kisasa wanahitaji jogoo bila hivyo mayai hayatagi kitu...
Kweli tunahitaji elimu sanaaaaaaaa
JAMANI DNA YANINI HAPO HEBU ANGALIENI HAO WATOT WANAVYOFANANA KAMA FOTO KOPI. PIA MSIMLAUMU MBUNGE LABDA MAMA MWENYEWE AMETAKA KWENDA KWA BABU. ILA AKITOKA KWA BABU SERIKALI IFUATILIE HILI JAMBO ASAIDIWE. INAWEZEKANA KWELI HUYU MAMA ANAPATA MIMBA KAMA TEGU KAMA ALIVYO SEMA MDAU HAPO JUU HII NI DUNIA JAMA
ReplyDeleteMhhh jamani, ni lazima mabingwa wa kina mama wawajibike kusaidia huyu mama ili ijulikane hasa ni nini kinaendelea katika mwili wake. Ni aibu kwa nchi nzima yenye wasomi kukaa kimya kwa jambo kama hili
ReplyDelete