Katibu wa Jumuiya ya Watanzania New York Mdau Vincent Mughwai (shoto) akiwa na rafikize Tony Mbimbi toka Sudan (kulia) na Sebastian Mhlanga toka Zimbabwe baada ya wote kula nondozzz za MA in Political Economy and Development chuo kikuu cha University of Bridgeport wikiendi ilopita
Mdau Vincent akiwa na kaka zake Alute (shoto) na Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki wakila pozi
Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu akitunukiwa International College Fellow Award na chuo hicho cha Bridgeport kwa harakati zake za ukombozi wa kisiasa na vita dhidi ya ufisadi
Mdau Vincent akiwa na wala nondozzz wenzie na profesa wao
Mdau akiwa katika picha ya pamoja na kaka zake, dada, binti na mama watoto wake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2011

    Mdau Vicent Nakukubali, Ila nina swali la kiufundi...Hiyo Nondo yako uliyokula unaileta TZ kutusaidia au unaendelea kuitumia hukohuko kwa Baba Mdogo Obama,...

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana kwa kazi nzuri, mheshimiwa Tundu karibu sana Houston kwani makamanda wengi hapa Houston wangelipenda uwape mwanga wa nini kinachi=ojiri kule Bongo naomba tuwasiliane ktk zuberi.hamisi@yahoo.com
    kwa ajili ya namba za simu na kila kitu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 09, 2011

    Mh. Tundu Lissu naomba upite hapa Houston. Wadau tupo willing kukufanyia mchakato mzima ukaja hapa hata kwa masaa machache, naomba utupatie namba yako hapa usa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2011

    Hongera sana Lissu. Jitihada zako za kutetea maslahi ya Taifa tunaziona. Tunaamini kuna siku tanzania itaondokana na uongozi uliojaa ubinafsi na kuna siku utawala wa sheria utachukua mkondo wake. Huo ndio utakuwa mwanzo wa safari ya maendeleo ya kweli Tanzania. Usikate tamaa. Wape Hi wapiganaji wenzako akina Halima Mdee, Wilbroad Slaa, Kabwe Zitto, John Mnyika na Mebere Marando.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 10, 2011

    Congrats. U have made it my brother.
    God bless you man.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 10, 2011

    Yaani hicho chuo kimetamka WAZI kuwa kinampa Tundu Lisu digrii ya kupambana na ufisadi? au ndiyo yale yale ya kutuambia kuwa Nizar Khalfan anachezea timu ya mabingwa wa marekani ya kaskazini wakati timu yenyewe ndio imeingia kwenye ligi mwaka huu

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 10, 2011

    Mdau umechemka, hakuna kitu kama chuo kikuu cha university.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 10, 2011

    Mengi tuataongea lakini Tundu Lissu mpeni haki yake. Anatetea maslahi kwa dhati na si kwa unafiki. Msiojua historia yake fuatilieni kesi ambazo amekuwa akisimamia. Karibia zote amekuwa akitetea wanyonge na haki iliweza kupatikana hata pale wenye mikono ya damu walipotaka kuingilia kati. Najua binadamu tuna hisia za wivu, chuki, udini, ukabila n.k. naomba tuziweke hizi pembeni pale tunapotaka kumhukumu mtu. Hicho chuo kimefanya vyema sana kumkumbuka mpiganaji kama huyu. Nadhani vyuo vingi hata vya hapa nchini vilitakiwa viwaenzi watu kama hawa kwa kuwapa tuzo pale wanapofanya mambo yenye maslahi kwa taifa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 10, 2011

    @ tue may 10.09:15:00AM wewe ndio umechemka
    vipo vingine vingi tu nikiorodhesha havitatosha nakupa hivi viwili vitakusaidia
    1.UWANJA WA KARUME STADIUM
    2.BARABARA YA MOROGORO ROAD
    upooooo au unakodoa macho kama mjusi kabanwa na mlango LOL

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...