meneja uhusiano mwandamizi wa benki ya Posta,Noves Moses (kushoto) akimkabidhi mkuu wa shule ya sekondari ya Bakoba, Methew Mabruk meza na viti vilivyotolewa na benki wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika shule hiyo.
meneja uhusiano mwandamizi wa benki ya Posta tawi la Bukoba, Noves Moses akisikiliza kwa makini wimbo wa shule uliokuwa ukiimbwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Bakoba, Bi Moses alikuwa shuleni hapo mwishoni mwa wiki kukabidhi msaada wa meza 50 na viti 50 vilivyotolewa na benki hiyo kwa shule hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5.



Safi sana Posta.Mimi nimesoma hapo 1986-1989 O-level.Shule iko hapo upande wa Pili wa Posta..Miaka ile kulikuwa hakuna kuvuja mitihani kama sasa.Ukifaulu umefaulu kweli na kihalali.tulikuwa tunashindana kufaulu kati ya Bukoba 'Seko',Kahororo,Ihungo,Nyakato na Rugambwa.Kipindi kile shule za serikali zilikuwa 'zinatesa' si mchezo
ReplyDeletena zilikuwa zinaheshimika sijui kumetokea nini hapa katikati.
D.Villa
Yaani hakuna sababu ya wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati. Million 4 madawati 50 na Viti 50? Gari moja inanunuliwa million 70. Kwanini tusijinyime wadogo zetu, watoto wetu, wajukuu zetu wakakaa kwenye madawati Kama sisi tulivyokua tukisoma? Hatuoni aibu? Kweli ntu unakwenda kutembelea shule na gari ya mamillioni na kuwaangalia wanafunzi machoni wakati wamekaa chini!!!! Ni nini serikali inalo la kujitetea kweli?
ReplyDelete