Mashindano ya ulimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Vodacom Miss Arusha City Center 2011 yanatarajiwa kuzinduliwa kesho Mei 2 katika ukumbi wa Via Via jijini Arusha.

Akizungumza na blog hili, mraribu wa shindano hilo Bi. Sophia Urio alisema kuwa kwa sasa wamejiandaa vyema tayari kwa ajili ya kufanya uzinduzi huo na mashindano hayo rasmi yatafanyika leo katika Ukumbi wa Triple A jijini humo.

Mpaka sasa wamehakamilisha wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo wenye mvuto na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha.

"Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni uzinduzi wa mashindano hayo ili tuweze kuendelea na kila kitu," alisema Bi. Sophia Urio.

Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.

Wadhamini katika shindano hilo ni Vodacom, Startimes, Stone, Shuphaa Quality boutique, Janeths Beaty Parlour pamoja na Africasana Pub iliyopo Holili, Moshi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...