Waziri wa Fedha na Uchumi, Mh. Mustafa Mkulo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, mjini Dodoma, kukanusha taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mh. Zitto Kabwe kwenye mkutano wa hadhara mkoani, Mbeya kuwa Serikali imefilisika na inakopa fedha kulipa mishahara wakati si hivyo na kwamba Serikali imewalipa mishahara wafanyakazi pamoja na wabunge, akiwemo Mh. Zitto Kabwe.
Home
Unlabelled
mkullo akanusha madai kuwa serikali imefilisika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Bwana Mkulo Serikali imefilisika. Tunaomba ukae kimya kabisa. kabla watu hawajarusha makombora hewani. Na wewe ni tatizo kubwa kabisa kwa serikali yetu na unafahamu hilo.
ReplyDeleteMichuzi naomba uichapishe hii koment kwa kuwa naamini imetoka kistaarabu na kwa kumheshimu mh waziri.
asante,
Mkullo,
ReplyDeleteumekuwa na kiburi cha kutukana hata wanaotupa hela, sasa leo umeambiwa ukweli na mheshimiwa mwenzako ndo unafikiria mambo ya uzalendo. Ungekuwa mzalendo ungesikiliza ushauri wa wataalamu wako hapo hazina, ungesimamia ukusanyaji wa mapato, ungejenga uchumi bora. Wewe unakopa hata benki za biashara...ni aibu tupu. hulipi mahitaji ya serikali kama mishahara nk...wakubwa wa nje wameshasema wewe ni waziri bomu. Hilo tunakueleza na ujirekebishe,...
Kwani serikali hamjui hiyo ni propaganda? Hongera Kabwe kwa propaganda hii. Propaganda inatumika kuchokonolea jambo ambalo kundi fulani lina mashaka nalo wakati huohuo kundi lingine limeamua kuficha ukweli huo. Kwa njia hii kundi liloficha siri litalazimika kuongelea hadharani kuhusu shutuma iliyotolewa. Na hapo ujumbe utakuwa umefika na ukweli utakuwa umebainika.
ReplyDeleteNASHANGAA SANA SERIKALI KUFICHA FICHA SIRI MWISHO WAKE UPO.WAFANYAKAZI WALICHELEWA KULIPWA MISHAHARA NI KWELI TATIZO WANAHABARI HAMNA TAARIFA NA KIONGOZI AKISEMA TU WOTE KIMYA.
ReplyDeleteZITO NI WAZIRI KIVULI WA FEDHA KWA HIYO ANAJUA MAMBO YA WIZARA YA FEDHA KWA HIYO NI NANI MUONGO KUONGELEA SUALA LA KUKOPA KWA SERIKALI.
NILISOMA GAZETI LA CITIZEN LIKIELEZA SERIKALI IMEAMBIWA ISIKOPE PESA KUTOKA NJE IPO KWENYE MSTARI MWEKUNDU SASA SERIKALI IMEKOPA MABENKI YA NDANI INAFICHA UKWELI.
NDUGU WANAHABARI NAOMBA MUWAELEWESHE WANANCHI KUHUSIANA NA SERIKALI KUWA NA MADENI MAANA WATOTO WETU WATAKUJA KUANGAIKA SANA BAADAYE KULIPA MADENI YA WAHESHIMIWA WALIYOYATUMIA KWA UFISADI
sasa hivi wahisani hawatoi tena pesa za bure..bajeti ya serikali inategemea asilimia 70-80 kutoka kwa wahisani. sasa yale mashangingi ya millioni 300 kila mbunge na watendaji wa kuu wa serikali unafikiri hizo pesa zitabaki tu.. inawezekana kweli kwamba serikali imeishiwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha. fedha zinatumiwa katika kujionyesha zaidi (mashangingi, ma lexus, majumba ya kifahari, masafari yasio na msingi) kuliko kujenga misingi ya uchumi.
ReplyDeleteTunaona kila jambo linalohusu jamii halitekelezwi na serikali lina subiri wahisani kama majengo ya shule, visima vya maji, barabara na pia mahospitali sasa tutegemee nini? viongozi wengi wa serikali hawajui wanapokwenda ili mradi siku iishe..na hii imetokana na kutupa kabisa umuhimu wa kushirikisha wasomi katika masuala muhimu ya kitaifa (uchumi, afya, jamii) na kuamua kufanya maamuzi kisiasa.
Anonymous wa May 10, 11:32:00AM, 2011 umeeleza ukweli kabisa. Kila jambo wanataka liamuliwe kisiasa. Matokeo yake hawawashirikishi wadau sahihi kama vile wanataaluma na matokeo yake ndio kama hayo. Aibu ziwapate kila kukicha lakini hamjifunzi. Wapo wachumi waliobobea nchi hii na wanaweza kutoa sababu za nchi kutokuwa na maendeleo na wanaweza kupendekeza mambo ya kufanya lakini wanaonekana kana kwamba hawana umuhimu. wakati mwingine serikali imekuwa ikiwashirikisha watu wacahache ili kukwepa lawama lakini wanaoshirikishwa hawana nguvu ya kufanya maamuzi. Watakachofanya ni kujitahidi kukubaliana na anavyotaka kiongozi. hatutafika kwa uongozi wa aina hii.
ReplyDeletehivi benki kuu haiwezi chapisha manoti mpaka mkakope nje?????
ReplyDeleteMimi namfuatilia zitto kwa karibu sana.habahatishi kabisa.hili la serikali kufilisika amechelewa kulitoa.serikali ilifilisika long taimu.wafanyakazi wa serikali wana hali mbaya sana.heshima imepotea kabisa kwa sababu ys maslahi duni.hspo hazina penyewehswajalipa madeni ya stahili za watumishi zaudi ya miezi mitano sasa.mkulo ameshindwa kusimamia ukusanyaji wamapato kupitia tra.tra imepoteza sifa yake.mkullo amekuwa na kiburi ya kuwakoromea hata watoa noti wslio hapo umoja house.sasa anawaza misaada badala ya kusimamia uchumi wa nchi.hamsikilizi hata makatibu wakuu na wataalamu wake...mkullo is disaster ti our govt.
ReplyDeletehivi mnaposema gari la milioni mia 3 kweli unalijua?au mnaropoka tu nyie wabongo mnaojifanya kila kitu mnajua?na wenzenu waliisha waona kuwa wajinga wanazidi kuwatumia tu?
ReplyDelete