Marehemu Happy Kulanga (kushoto ) enzi za uhai wake akipokea cheti chake katika moja kati ya mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira (JET)
Safari ya mwisho ya mwanahabari wa gazeti la Mtanzania mkoa wa Ruvuma Happy Kulanga.
Mazishi ya mwanahabari Happy Kulanga leo
Mwanahabari Francis Godwin (kushoto) akitoa salama za rambi rambi kutoka Ruvuma Press Club na toka Gazeti la Mtanzania ambalo marehemu alikuwa akilifanyia kazi kama mwandishi mkoa wa Ruvuma
jamani poleni ruvuma.
ReplyDeletePoleni familia na kazini kwa marehemu.
ReplyDeleteNinachoipendea bongo huwezi kujua dini ya mtu kwa jina tuu.
Hii ni hatua kubwa duniani kuliko nchi zote hasa zenye kujidai zina usawa lakini zikiwa na udini kisirisiri.
Kwa hapo upo sahihi kwani hata marehemu Komredi Moses Nnauye (Baba yake Nape Nnauye wa CCM) alikuwa ni muislamu ingawa hakuna aliyefahamu hadi siku ya kuzikwa kwake. Ingawa hata hivyo usisahau kwamba hapo zamani tabia hii ilikuwapo kutokana na watu kuogopa kubaguliwa hasa katika mashule na makazini kutokana na misingi ya dini zao, wapo wengi mno na sina haja ya kuwataja kwa majina, na mbaya zaidi wengi walifelishwa mashuleni kwa sababu tu ya majina regardless how intelligent they were!!!
ReplyDeleteKama inafikia watu kubadilisha majina ili kuepuka ubaguzi basi serikali imelala saana au ni lengo la baadhi ya wakuu serikalini kwa makusudi kisirisiri.
ReplyDeleteKatiba ya sasa inatakiwa kujibu hili ili watu woote wawe huru kukaa na majina yao bila kuadhibiwa kielimu, kijamii, kirafiki, kikazi, kisheria, kihuduma, kibiashara n.k.