
Ni shangwe tu jioni hii ndani ya ukumbi wa Mawingu Club,uliopo katikati ya jiji la Arusha,ambapo hivi sasa linaendelea shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta freestyle 2011.Ama kwa hakika ni shindano ambalo limekuwa na msisimko mkubwa kwa wakazi wa jiji la Arusha.Wamejitokeza washiriki 30 lakini anaetakiwa kuwa kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti fiesta freestyle ni mmoja tu.
Ni bato tu kihip hop kwa kwenda mbele jioni hii,kila mmoja anaonyesha anaonesha umahiri wake wa kukamua mashairi awezavyo.
Baadhi ya mashanbiki wakifuatilia mpambano huo ulijaa msisimko mkubwa jioni ya leo ndani ya ukumbi wa Mawingu Club.
Mmoja wa washiriki wa hip hip akichana jioni hii kwenye shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta freestyle 2011.

Meneja wa kinywaji cha Serengeti Primeum Lager,Allan Chonjo akitoa mwongozo kwa mwendesha shughuli nzima ya kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti fiesta freestyle jioni hii ndani ya Mawingu Club, Ruben Ndege a.k.a Ncha Kali ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds FM.

Mmoja wa wakali wa muziki wa hip hop ndani ya Bongo Fid Q ambaye ni mmoja wa majaji akizungumza jambo wakati wa kuanza shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu na serengeti fiesta freestyle 2011 ndani ya Mawingu Club jioni hii,kushoto ni jaji mwingine aitwaye Noise Maker.

Baadhi ya Wakazi wa jiji la Arusha wakiwa ndani ya ukumbi wa Mawingu Club uliopo katikati ya jiji ,wakishuhudia shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011,shindano hili linaenndelea hivi sasa limejaa msisimko mkubwa,hasa ukizingatia jiji la Arusha lina vijana wengi wenye vipaji vya kufoka foka a.k.a hip hop. Picha na Jiachie




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...