Miss Universe 2011,Nelly Kamwelu akiwani mwenye furaha mara baada ya kushinda usiku huu katika mashindano yaliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar.
Miss Universe 2011,Nelly Kamwelu (kati) akiwa na mshindi wa pili,Neema Kilango (kulia) na Mshindi wa tatu,Yaceba Asenga mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Miss Universe 2011 yalifofanyika katika hoteli ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar usiku huu.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania,George Rwehumbiza (kulia) na Meneja wa Mambo ya Nje wa Vodacom,Nector Foya wakiwa katika picha ya pamoja na Miss Universe usiku huu.
Miss Universe 2010 aliemaliza muda wake usiku wa leo,Hellen Dausen akimvisha Crown Miss Universe 2011,Nelly Kamwelu ikiwa ni ishara na kukabidhima rasmi majukumu hayo ya ulimbwende.
Top 5 (anaekatika katikati yao ni MC Abby)
Mratibu wa shindano la Miss Universe,Maria Sarungi akitangaza washindi katika kinyang'anyiro hicho.
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation ambaye pia alikuwa ni mmoja wa majaji wa mashindano hayo,Mwamvita Makamba akiuliza swali kwa mmoja wa washiriki wa Miss Universe wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji.
Kwa kuona picha nyingi zaidi,


 Mwandishi Wetu
 Mlimbwende  Nelly Kamwelu ameibuka mshindi wa mashindano  ya Miss Universe Tanzania baada ya kuwashinda wenzake 18, Katika mashindano yaliyofanyika kwenye hotel ya Golden  Tulip jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.

Haikuwa kazi rahisi kwa mrembo huyo kuibuka na taji  hilo kwani  kulikuwa  na ushindani mkubwa.  Kutokana na ushindi huyo, Nelly ambaye alishiriki Miss  Tanzania mwaka 2008,  na kushindwa kufanya vyema, ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa  yaliyopangwa kufanyika nchini Brazil Septemba.

 Hali ilikuwa tofauti kwa Nelly baada ya Chifu Jaji Maria  Sarungi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Compass Communications  kumtangaza mshindi. Hii inatokana na ushindani ulipo kati yake na Neema Kilango  na Yacoba Assenga ambao walikuwa tishio tokea kuanza kwa  mashindano hayo.

 Nelly ambaye alijikita katika urembo mwaka 2008 na kushika  nafasi ya pili katika shindano Miss Ilala na Miss DarCity  alisema kuwa anashukuru kwa kuwaa taji hilo kwani pamoja na  kushinda amekiri kuwa ushindani ulikuwa mkali.

 “Namshukuru Mungu kuibuka ushindi katika mashindano haya, ndoto yangu imetimia, naahidi kufanya vyema katika  mashindano ya kimataifa,” alisema Nelly.
 Baada ya ushindi huo, Nelly alijinyakulia kitita cha  shilingi Milioni 3 na kupata Schoralship ya kwenda kusoma  nchini Marekani katika chuo cha New York Film Academy ambapo  atachukua kozi ya Mawasiliano ya Umma “Mass
 Communications” na utengezaji wa filamu.

 Mbali na zawadi hizo pia alijinyakulia simu ya Blackberry  kutoka mtandao wa  Jamii Forum, tiketi tatu za ndege  kwa ajili ya safari za kufanya kazi za jamii kutoka   Precision Air, vipodozi vyenye thamani ya shilingi 350,000  kutoka Shear Illusion na mafunzo ya mwaka mmoja  yatakayotolewa  na Mercy G Beauty ambao wote ni  wadhamini.

 Neema Kilango alishinda nafasi ya pili na kupata sh.  Milioni 1 na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika  mashindano ya Miss Earth nchini Thailand.  Neema pia alishinda taji la Miss Congeniality na kupata ofa  ya kusoma masomo ya ujasiliamali yenye thamani ya dola 1,500  za kimarekani.

 Yacoba Assenga aliibuka mshindi wa tatu na kuzawadiwa sh. 500,000 na kushinda nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika  mashindano ya Miss International.  Vile vile Linda Deusaliibuka na taji la Miss  Entrepreneurial Mind set  na kupata ofa ya kusoma maomo  ya Ujasiliamali yenye thamani ya dola 1,500 za kimarekani.

 Mashindano ya Miss Universe yalifanyika kwa mara ya kwanza  mwaka 2007 ambapo Flaviana Matata aliibuka mshindi sambamba  na kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa  yaliyofanyika nchini Mexico.

 Flaviana ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, aliingia  hatua ya 10 bora (nusu fainali) na baadaye Amanda Ole Sululu  aliiwakilisha Tanzania mwaka uliofuata na kufuatiwa na  Illuminata James na mwaka jana Hellen Dausen.
 
Mbali ya Mwananchi Communications Limited (MCL), wadhamini  wengine wa mashindano ya mwaka huu ni Vodacom Tanzania,  Golden Tulip, Chanel Ten, Magic FM, The Citizen, Precision  Air, Coca Cola, Dar Life,  Jamii Forums, MH Gallery,  Dodoma Hotel, Triple A,  Vayle Springs, New York Film  Academy na Shear Illusion.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2011

    Neema Kilango ndio alitakiwa kuchukua, kweli bongo tuna wadada wa zuri can't wait kuja kuoa nyumbani.. nawapenda wadada wa nyumbani japokuwa sifa zenu ninazozipata ni mbaya kwenda mbele

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2011

    Kwanza kabisa kina dada kwakweli wamependeza, hongera kwa mshindi.

    Pili mimi nina swali au lalamiko na ikiwezekana wadau mtanikosoa. Kusema ukweli sipendi kabisa jinsi wanaume wa kibongo (sio wote but for the most part) tunavyovaa. Au nisema bado hatujajua nini cha kuvaa kutokana na shughuli. Mfano angalia hapo juu ndugu yangu George alivyotoka na shati lake (it doesn't matter linacost kiasi gani) huamini kwamba amekuja kwenye shughuli muhimu.

    Sasa angalia kina dada? mwalaaaa...wameulamba.

    Nimeona mara kibao watu wanaenda Ikulu kuonana na Rais wamevaa kandambili, kitambi kikubwa lakini chini kaweka kandambili. Kweli wadau inakuja hiyo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2011

    HONGERA SANA MABINTI WOTE WASHINDI. ASANTE MARIA SARUNGI KWA KUENDELEZA FANI HII. BW. GEORGE RWEHUMBIZA - UNATUANGUSHA - JITAHIDI MAVAZI BASI HASA KATIKA SHUGHULI KAMA HIZI ZA FASHION NA MODEL KAMA WENZAKO HAO MAJAJI WALIVYO SOPU SOPU.
    Alex bura, dar

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2011

    Jamani mie naomba ufafanuzi, kuwa iwapo huyu mshindi ana umri wa miaka 18 mwaka huu 2011 na mwaka 2008 alishiriki mashindano ya umiss alikuwa na umri gani wakati huo? Na kwa hesabu ya haraka haraka hapo kati ya 2011 na 2008 kuna tofauti ya miaka 3 je alikuwa na miaka 15 na kama kweli watoto wanaruhusiwa kushiriki mashindano ya umiss siku hizi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2011

    With all respect, Maria Sarungi is so beautiful.

    ReplyDelete
  6. Nawapongeza mabinti wote walioshiriki katika Miss Universe Tanzania. Itakuwa safi kama Miss Universe wetu atafanikiwa kuingia katika Top 10 katika mashindano ya Miss Universe kama Flaviana Matata alivyofanya mwaka 2007.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2011

    wewe anony hapo juu umetoa wapi hiyo miaka 18? soma vizuri article kabla hujaanza malalamiko! article imesema amewashinda wenzake 18 na sio kwamba huo ni umri wake. No wonder watu wanafeli mitihani kwa kurukia kujibu kabla ya kusoma na kuelewa swali..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...