Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen ataingoza timu hiyo kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) itakayochezwa Mei 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 12 kamili jioni.

Awali Poulsen ambaye pia ni mkufunzi wa makocha alikuwa ameteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuendesha kozi ya makocha nchini Gambia kuanzia Mei 6- 14 mwaka huu. Kozi hiyo imeahirishwa hadi Septemba mwaka huu.

Kikosi cha wachezaji 19 wa Stars kinaingia kambini kesho (Mei 7 mwaka huu) hoteli ya Atriums jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayo inazikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza.

Wachezaji walioitwa na Poulsen kwa ajili ya mechi hiyo ni makipa Shabani Kado (Mtibwa Sugar), Shaaban Dihile (JKT Ruvu) na Juma Kaseja (Simba). Mabeki ni Shadrack Nsajigwa (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Juma Nyoso (Simba) na Kigi Makasi (Yanga).

Viungo ni Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Jabir Aziz (Azam), Ramadhan Chombo ‘Redondo’ (Azam) na Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).

Washambuliaji ni Machaku Salum (Mtibwa Sugar), Mrisho Ngasa (Azam), Mohamed Banka (Simba), John Bocco (Azam) na Mbwana Samata (Simba).

Wachezaji wanaocheza nje ambao wataanza kuripoti wiki ijayo ni Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden).

Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2011

    Mr. Wambura unafanya kazi nzuri,angalau unatu-update na kinachoelendelea.Tunategemea Kocha wetu atawatumia wachezaji ambao hawapangwi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza kwenye mechi hii nao waweze kuonyesha uwezo wao..ni mawazo yangu Bwana Bon.Jitahidini hao 'mapro' wetu wafike kwa ajili ya mechi ya Bangui mwanzoni mwa June.ile ndiyo mechi itakayoamua hatima yetu.

    David V.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...