Mheshimiwa Jaji Mkuu;Wazee Wetu, Mzee Cleopa Msuya na Mzee Pius Msekwa; Ndugu Mawaziri; Ndugu Naibu Mawaziri; Ndugu Makatibu Wakuu; Ndugu Naibu Makatibu Wakuu;Wakuu wa Vyombo vya Dola;Wageni Waalikwa;Mabibi na Mabwana:
Ukaribisho
Nianze kwa kuwakaribisha nyote kwenye Semina Elekezi inayojumuisha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu. Kama lilivyo jina lake, Semina hii ni ya kuelekezana juu ya namna tutakavyotimiza majukumu yetukatika Serikali. Tulikuwa na Semina kama hii mwaka 2006. Imetusaidia kupata mafanikio tuliyoyapata miaka mitanoiliyopita. Naamini na Semina hii itatusaidia kupata ufanisi tunaoutarajia na ambao wananchi wanautarajia kutoka kwetu.
Ndugu Viongozi na Watendaji wa Serikali;
Niruhusuni niombe radhi kwa niaba ya Viongozi Wakuu wawili kutokuwa nasi siku ya leo. Wa kwanza ni Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wa pili ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali MohamedShein. Makamu wa Rais yuko Uturuki kuniwakilisha katika LDC Summit. Mwanzoni nilikubali kushiriki kwenye LDCSummit, lakini baada ya tarehe za Semina yetu kubadilika na kuangukia kwenye tarehe za Mkutano huo nikawa sina namnaila kutuma mwakilishi.Kwa uzito wa mkutano wenyewe na matumaini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na wenyeji wetu kuhusu ushiriki waTanzania nikaona Makamu wa Rais atuwakilishe. Makamu wa Rais amefuatana na Mheshimiwa Prof. Anna Tibaijuka, Waziriwa Ardhi na Maendeleo ya Makazi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa MahadhiJuma Maalim. Najua watakosa uhondo, lakini tutawapatia DVD ya Semina wataona na kusikia tuliyozungumza. MheshimiwaRais wa Zanzibar amebanwa na vikao vya maandalizi ya bajeti.
Madhumuni ya Semina
Ndugu Viongozi,
Katika Semina hii majukumu ya msingi ya Serikali ya utawala, maendeleo na ulinzi na usalama yatafafanuliwa. Pia itaelezwa jinsi kila mmoja wetu anavyohusika nayo na anavyotegemewa kutimiza wajibu wake. Katika hotuba yangu ya kuzinduaBunge nilitaja malengo 13 ambayo yamejumuisha mambo makuu tutakayoyapa kipaumbele katika Serikali katika miakamitano hii. Lakini nilikumbusha kuwa yale mambo 13 ni muhtasari wa maelekezo yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi yaChama cha Mapinduzi.
Ndugu Mawaziri;
Mtakumbuka kuwa katika mkutano wangu wa kwanza nanyi niliwasisitizia umuhimu wa Ilani ya Uchaguzi kwa kila mmojawenu na kwa Serikali yetu kwa jumla. Niliwaambia kuwa Ilani ndiyo mkataba mkuu baina ya Chama cha Mapinduzi nawananchi. Utekelezaji wake ndicho kipimo kikuu cha uwezo wetu wa kuongoza, mwaka 2015. Niliwataka kila mmoja wenuatambue ukweli huo na kutengeneza mkakati wa kutekekeleza Ilani kwa yale mambo yanayohusu Wizara yake. Sina shakakuwa takriban miezi mitano baadae kila mmoja wetu atakuwa amekamilisha kazi hiyo na kuingiza katika mipango ya kazi yaWizara itakayotekelezwa kuanzia bajeti itakayowasilishwa Bungeni mwezi ujao.
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Siku ile pia nilisisitiza jambo kwa Mawaziri ambalo napenda kulirudia tena leo kwani linawahusu na Makatibu Wakuu. Ninyikwa pamoja, Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu ndiyo timu moja ya uongozi na utawala katikaWizara. Kama viongozi mnategemewa kuonyesha njia kuhusu nini cha kufanya kutekeleza majukumu ya Wizaranilizowakabidhi kuziongoza.Katika jukumu lenu la utawala mnategemewa kuwa makini na mahiri katika kutumia rasilimali watu, vifaa na fedha za ummamlizokabidhiwa katika kutekeleza majukumu yenu. Mnategemewa kuwa na mipango na mikakati thabiti ya kutekelezamajukumu hayo.
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Katika Wizara kila kitu huanzia na kuishia kwenu. Hakuna mwingine tena kuliko nyie isipokuwa mamlaka zilizo juu yenu;yaani Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais. Kwa sababu hiyo, ili muweze kutimiza kwa ukamilifu wajibu wenu huohamna budi kwanza kabisa kutambua vyema majukumu yenu na jinsi ya kuyatekeleza. Semina hii ina shabaha ya kusaidiakatika hilo. Lakini, njia kubwa zaidi ni ile niliyowaambia siku ile, yaani ninyi wenyewe kufanya bidii ya kujua kwa kusoma,kuona na kufanya shughuli za Wizara zenu kwa makini.Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu mnatakiwa kuyajua kwa kina mambo yote yanayohusu Wizaramnazoziongoza. Vinginevyo hamtaongoza vizuri. Mtakuwa wababaishaji. Mtashindwa kutoa malengo maana mtakuwahamjui nini cha kuekeleza, mtashindwa kusimamia mambo, kwa vile hamjui cha kusimamia, mtakuwa hamuonekani mkifanyachochote cha maana kwa sababu hamna jambo la kufanya zaidi ya mambo ya kawaida – routine issues
. Mawaziri na Makatibu Wakuu lazima mtoke. Hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kujua mambo yahusuyo Wizara yenu na ndiyo njia bora yakuongoza: kuona wenyewe na kutenda. Itawafanya mjiamini kuelekeza na pia mnaposimama mbele za watu na kusema.Msiwe mangimeza. Tokeni, tembeeni kuona shughuli zenu. Tembeleeni wananchi muwafahamu, wawafahamu, mjue shidazao muwatatulie.
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Ili mjue mambo ya Wizara zenu vizuri lazima mtengeneze utaratibu mzuri wa kupashana habari kuhusu mambo yanayotokeaWizarani. Utaratibu utakaomwezesha kila mmoja kujua kinachoendelea Wizarani. Msipofanya hivyo kuna hatari ya ninyiwenyewe viongozi wakuu mkawa hamjiamini na hata kuwa na kauli tofauti kwa jambo hilo hilo. Mmoja anasema hivi namwingine anasema vile. Kuna hatari ya kuzuka kutokuelewana miongoni mwenu.Hii pia ni muhimu sana hasa kwa sababu barua huandikwa kwa Waziri au Katibu Mkuu. Msipotengeneza utaratibu wakupashana habari Waziri anaweza asijue anachojua Katibu Mkuu na kinyume chake. Na, baya zaidi Naibu Waziri na NaibuKatibu Mkuu wanaweza kuwa gizani kabisa. Naibu Waziri hushikilia Wizara anaposafiri Waziri na ndiye msemaji wa Wizarakatika Bunge asipoyajua vyema yanayotokea au mambo yanayohusu Wizara hatakuwa msemaji mzuri na wa kujiamini waWizara. Naibu Katibu Mkuu hushikilia ofisi ya Katibu Mkuu anapokuwa hayupo. Hatafanya kazi kwa kujiamini naatashindwa kuamua mambo kwa sababu hana habari ya mambo yanayohusu Wizara. Mambo yatakawia na mengine kukwamakwa sababu hiyo.Pamoja na kutoa fursa kwa kila mmoja wenu kuona na kujua kinachotokea Wizarani, jengeni utaratibu wa kukutana mara kwamara kuzungumzia shughuli za Wizara zenu. Itasaidia sana. Ndiyo maana Jeshini kuna Officers Mess kutoa fursa ya maofisakufahamiana na kuzungumza masuala yahusuyo shughuli zao. Mnaweza kuwa na vikao vya mara kwa mara au hata kunywachai pamoja. Hata nyie mnaweza kuwa na utaratibu kama huo.
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Narudia kuwakumbusha kwamba msingi wa utendaji Serikalini ni katiba, sheria, kanuni na taratibu. Ni muhimu kwenu kamaviongozi mkajielimisha juu ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi katika sehemu zenuza kazi. Uhalali wa maamuzi mtakayoyafanya hupimwa na sheria. Ukifanya maamuzi yanayokinzana na sheria utahojiwawewe binafsi lakini pia utaibebesha Serikali mzigo wa hasara na fedheha itakayotokana na maamuzi hayo.Lakini pia maamuzi yasiyofuata sheria yanaweza kuwa na madhara kwa wananchi. Heshimuni Katiba na fuateni sheria,kanuni na taratibu zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yenu. Katika semina hii masuala hayo yatafafanuliwa nakuzungumzwa. Kadhalika uhusiano wa Serikali na mihimili mingine ya dola yani Bunge na Mahakama utafafanuliwa.
Uwajibikaji kwa Wananchi
Ndugu Viongozi;
Lazima tukumbuke kwamba Serikali yetu imewekwa madarakani na wananchi kwa ajili yao na siyo kwa ajili ya viongozituliopo madarakani. Serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia na kutatua matatizo yanayowakabili wananchi na kuwaleteamaendeleo. Wananchi wanapenda kuona Serikali yao ina viongozi na watumishi waadilifu, wachapakazi hodari,wanaowasikiliza, wanaojali shida zao na wepesi wa kushughulikia na kutekeleza maamuzi mbalimbali ya Serikali. Ni wajibuwetu kama viongozi wakuu na watendaji wakuu kutimiza matarajio hayo ya wananchi.
Kuisemea Serikali
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Moja ya mada ya semina hii inahusu mawasiliano ya Serikali. Kwa maneno mengine kuisemea Serikali. Hili ni jamboambalo tuna udhaifu mkubwa. Sijui kwanini hatuwi wepesi kuyasemea mafanikio mengi tuliyoyapata tukaacha wasiotutakiaheri wanaosema hatukufanya kitu wasikike mpaka waonekane wanasema kweli. Mwanazuoni mmoja bingwa wa habarialiwahi kusema kuwa “
kufanya kitu bila kuufahamisha umma ni sawa kama kitu hicho hakijafanyika
.” Mwingine anasemakuwa uongo ukisemwa mara nyingi hugeuka kuwa ukweli.Uzoefu wa miaka mitano umeonyesha kwamba tumefanya mambo mengi lakini wananchi hawakuelezwa ipasavyo. Pia,tumeacha upotoshaji kufanywa bila ya kusahihishwa au kuchelewa sana kusahihishwa. Hivyo basi, wananchi wamekuwawakijikuta wakiamini uongo na kulaumu au hata kuichukia Serikali kwa mambo ambayo ni potofu. Wangeambiwa ukwelimapema hawangefikia hapo. Lazima upungufu huo tuondokane nao. Lazima tuwe makini na hodari kuelezea shughulizinazofanywa na Serikali, mafanikio yanayopatikana na changamoto zilizopo.Aidha, tuwe wapesi kusahihisha upotoshaji wowote unaofanywa dhidi ya Serikali. Kutokufanya hivyo kumetugharimu sana.Hatuwezi kuendelea hivi wakati ninyi viongozi mpo, watu Mawizarani wapo, rasilimali zipo na vyombo vya habari vipovinasubiri kupewa habari.
Ukuzaji Uchumi na Maendeleo
Ndugu Viongozi;
Nilieleza awali kuwa mojawapo ya majukumu ya msingi ya Serikali ni kuleta maendeleo ya nchi na watu wake. HususanSerikali inalo jukumu la kukuza uchumi na kuwapatia wananchi huduma za msingi za kiuchumi na kijamii kwa lengo lakuongeza mapato na kuboresha hali ya maisha ya Watanzania. Hii ni kazi ya msingi sana kwa Serikali kufanya na lazimakufanikiwa. Kazi hiyo ndiyo moja ya sababu na shabaha pana ya Serikali kuwepo na sisi wote kuwapo. Kwangu mimi naninyi wenzangu kuleta maendeleo na kukidhi matumaini ya Watanzania ni changamoto na mtihani wetu mkubwa sana.Katika Semina hii masuala ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo yamepewa nafasi ya kuzungumzwa kwa upana. Pamoja nawatoa mada wa ndani, tunawashukuru marafiki zetu wa Benki ya Dunia kwa kutuletea mabingwa wa uchumi na maendeleokuja kuzungumza nasi. Naamini uzoefu na mifano ya nchi mbalimbali kuhusu kufanya mageuzi ya kiuchumi na kujileteamaendeleo kutatusaidia kuimarisha na kuboresha hatua tunazochukua nchini.
Ndugu Viongozi;
Hakika tumefanya mengi na mafanikio yanaonekana, lakini tunayo kazi kubwa sana mbele yetu ya kufanya. Tanzania nimiongoni mwa nchi 49 maskini sana duniani. Shabaha yetu kubwa ni kutoka hapa tulipo sasa na kuwa nchi ya uchumi wakati ifikapo mwaka 2025. Yaani, tutoke kwenye pato la wastani la USD600 la sasa hadi pato la USD1,500
mpaka USD3,000 mwaka huo. Niliamua na kuelekeza kuwa yafanyike mapitio ya
Vision 2025 na tuigawe miaka 15 iliyosalia katika mafungu matatu yamiaka mitano mitano. Tuwe na mipango ya maendeleo ya miaka mitatu tukianzia na huu unaowiana na kipindi chetu chauongozi. Hii itatuongoza vizuri zaidi kuelekea na kufikia lengo. Kazi ya mapitio inaendelea kama ilivyo ile ya matayarishoya mpango wa kwanza wa maendeleo. Katika Semina hii tutapata maelezo ya awali ya kazi inayoendelea.
Ndugu Viongozi na Ndugu Washiriki;
Tunao pia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) ambao tumekuwa tunautekeleza tangu mwaka2005. Tumekamilisha MKUKUTA I na hivi sasa tupo kwenye utekelezaji wa MKUKUTA II ambao utakamilika mwaka 2015.MKUKUTA umetusaidia sana katika kuainisha maeneo ya kipaumbele katika bajeti. Kwa ajili hiyo, imesaidia katika jitihadaza Serikali za kupunguza umaskini na kuinua hali ya maisha ya Watanzania. Bila ya shaka tutapata nafasi ya kuelezwamaudhui ya MKUKUTA II ili tuelewe namna ya kuwianisha shabaha zake na shughuli tunazozifanya katika Wizara zetu.
Ndugu Mawazirina Ndugu Makatibu Wakuu;
Kuinua hali ya maisha ya Watanzania kuna sura mbili: upande mmoja kuna kuongeza kipato chao. Yaani wasiokuwa nashughuli wapate shughuli za kufanya (kukuza ajira) na wale wenye shughuli zikue na kuimarika ili mapato yao yaongezeke.Mazungumzo yahusuyo kukuza uchumi yatatoa fursa ya kuyajadili mambo haya. Upande wa pili unahusu upatikanaji wahuduma za kiuchumi na huduma za kijamii zilizo bora na zinazotosheleza mahitaji. Wananchi wanataka kuona miundombinuhasa ya barabara zinajengwa na kuimarishwa, umeme wa uhakika pamoja na huduma za maji, afya na elimu zinapatikana kwakiwango kinachokidhi mahitaji na ubora unaostahili.Tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kuongeza upatikanaji wa huduma hizo katika miaka mitano hii. Lakini, kazi iliyo mbele yetu bado ni kubwa. Upande mmoja bado tunayo kazi ya kuwafikia wale ambao huduma hizo hazijawafikia. Na, upandemwingine tunayo kazi ya kuhakikisha ubora na uendelevu wa huduma pale inapopatikana. Kuyafanya hayo ni wajibu wamsingi wa Serikali, kinachotakiwa ni kujipanga vyema kwa mipango na rasilimali watu, vifaa na fedha ili kutimiza wajibuhuo.
Mapato na Matumizi ya Serikali
Ndugu Viongozi;
Uwezo wa Serikali kutekeleza majukumu yake unategemea sana kuwepo kwa rasilimali fedha na jinsi fedha hizozinavyotumika. Upatikanaji wa rasilimali fedha unategemea ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Serikali inapatamapato yake kupitia kodi na tozo mbalimbali. Kodi ndicho chanzo kikubwa cha mapato ya Serikali na chombo kikubwa chaukusanyaji wa mapato hayo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Katika miaka mitano hii mafanikio makubwayamepatikana na mapato yameongezeka karibu mara tatu kutoka shilingi 177 bilioni kwa mwezi hadi shilingi 430 bilioni kwa mwezi hivi sasa.Pamoja na nyongeza hiyo bado tunao uwezo wa kuongeza zaidi. Kuna watu wengi ambao bado hawajafikiwa na wigo wakodi. Laiti wangefikiwa mapato ya Serikali yangekuwa makubwa zaidi ya ilivyo sasa. Tutafanyaje tufanikishe hilo nichangamoto yetu sote Serikalini. Tufanye nini ili tuzibe mianya inayovujisha mapato ya Serikali ni swali ambalo sote katikaSerikali hatuna budi kutoa jibu muafaka. Kwa upande wa tozo mbalimbali karibu kila Wizara inazo tozo za namna hiyo.Wengi wenu hamjafikia hata theluthi moja ya malengo. Tutafanyaje ili tufikie malengo na kuyavuka ni swali ambalo kilammoja wetu anatakiwa kujiuliza na kutoa majibu sahihi.
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Sote tunajua kuwa licha ya tozo na kodi, chanzo kingine cha mapato ya Serikali ni mikopo na misaada kutoka Mabenki,Mataifa Rafiki, na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa. Tumepata misaada na mikopo mingi ya kutoka nje katika kipindikilichopita na muelekeo ni kuwa tutaendelea kupata zaidi katika miaka mitano ijayo. Tunatambua haja na hoja ya kupunguzautegemezi wa misaada na mikopo kutoka nje kwa kuongeza mapato yetu ya ndani. Katika miaka mitano hii tumeendeleakupunguza utegemezi lakini nia yetu sote iwe kupunguza zaidi. Naamini tutafika kwenye shabaha hiyo iwapo tutaongezamapato ya ndani. Naomba tuzungumzie namna ya kufikia shabaha hiyo.
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Usimamizi wa matumizi ya fedha tunazokusanya kama mapato ni jukumu jingine kubwa kwetu sote. Tuna wajibu wakuhakikisha kuwa fedha za walipa kodi zinatumika ipasavyo kuwaletea maendeleo wananchi. Katika kudhibiti matumizi nimuhimu kuelewa na kusimamia sheria, taratibu na kanuni za fedha na manunuzi ya umma kwa ufanisi wa hali ya juu. Taarifaza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zinaonyesha kuongezeka kwa ubora lakini bado tunayo kazi ya kufanyakufikia kiwango cha kusema sasa tunapumua. Bado kuna makosa mengi katika kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zamapato na matumizi ya fedha za umma. Nataka tuzungumze kwa dhati tutafikaje kwenye ufanisi wa hali ya juu kwenye eneo hilo. Hali hii hatuwezi kuiacha iendelee kuboreka kwa kasi ndogo iliyopo sasa.Viongozi na watendaji wakuu wa Serikali, mnatakiwa kuwa mfano kwa wafanyakazi mnaowaongoza kwa kuzingatia nidhamuya matumizi ya fedha za umma. Hakikisheni bajeti hazikiukwi, fedha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sheria nakanuni za fedha zinaheshimiwa. Niliagiza Kamati za Fedha ziundwe katika kila Wizara na Idara za Serikali zinayojitegemea.Je zimeundwa? Je zinafanya kazi? Hakikisheni zipo hai na zinatimiza wajibu wake. Zitasaidia sana kwa upande wakuongeza mapato na kudhibiti matumizi katika Wizara.
Ulinzi na Usalama
Ndugu Mawaziri na Ndugu Makatibu Wakuu;
Katika semina hii tutapata nafasi ya kuzungumzia masuala ya ulinzi na usalama. Tutawasikiliza Wakuu wa Vyombo vyaUlinzi na Usalama kuhusu usalama wa nchi. Pia tutamsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuhusu mapambano dhidiya rushwa na Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi kuhusu uadilifu wa viongozi.
Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru
Ndugu Viongozi;
Kama mnavyofahamu mwaka huu tunaadhimisha miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tumeazimia kusherehekea sikuhii kwa uzito unaostahili. Niliagiza tufanye mambo kadhaa muhimu ambayo ni pamoja na kufanya tathmini ya kina yamafanikio tuliyoyapata, katika juhudi zetu za kujiletea maendeleo. Aidha, niliagiza Wizara, idara na taasisi za Serikali nahata sekta binafsi zifanye tathmini ya shughuli zao na kuandika vitabu ili kuhifadhi kumbukumbu hizo muhimu kwetu na kwavizazi vijavyo.Vile vile niliagiza yafanyike maonesho maalum katika Uwanja wa Maonyesho wa Julius Nyerere hapa Dar es Salaam na kotemikoani kwenye viwanja vya maonesho, kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali katika miaka 50 tanguUhuru wa Tanzania Bara. Kwa kuwa tunakaribia nusu ya mwaka huu, ni vema sasa kukumbushana kuendelea na maandaliziya sherehe hizo. Ni matumaini yangu kwamba kila Wizara inakaribia kukamilisha tathmini hiyo. Walio nyuma sanawaongeze kasi. Tuliazimia pia kuwa tuanzishe mchakato wa kuipitia Katiba yetu. Tumeanza, lakini kuna upotoshaji mkubwa,lakini wajibu wetu sote tuliopo hapa kukabili hila na njama hizo chafu. Naamini tutafika salama. Kinachotakiwa nimshikamano na umoja miongini mwetu.
Hitimisho
Ndugu Viongozi Wenzangu,
Ni matumaini yangu kwamba maneno haya ya utangulizi niliyosema, yatatupatia msingi wa tafakuri katika mijadala namafunzo tutakayopatiwa katika siku nne zijazo hasa katika maeneo makuu ya semina ambayo ni pamoja na mfumo wautawala na utendaji; uchumi na maendeleo; utawala bora; ulinzi na usalama; muungano; na masuala mtambuka. Nimeambiwa kwamba semina hii itaendeshwa kwa utaratibu wa mihadhara kwa ajili ya kuwasilisha mada pamoja namajadiliano ya pamoja. Pia nimearifiwa kuwa kutakuwepo majadiliano katika vikundi ili kuchambua kwa undani zaidi madazilizowasilishwa. Hivyo, rai yangu kwenu nyote muwe tayari kushiriki kwa ukamilifu katika majadiliano kwenye mihadharakwa ukweli na uwazi bila kujali tofauti ya nyadhifa zenu. Wote muwe huru kutoa maoni yenu. Ndiyo maana tuko hapa.
Ndugu Viongozi,
Nawashukuru watoa mada waliokubali kuchangia ujuzi na uzoefu wao nasi. Baada ya kusema hayo sasa napenda kutamkakwamba Semina Elekezi kwa Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefunguliwarasmi

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...