
Ni kijana wa makamo hivi ambaye alionyesha kipaji cha kufreestyle kwa kiwango cha juu kabisa,anaitwa Rota Flavian Komba ndiye aliyeibuka kinara wa msimu wa dhahabu wa unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011 ndani ya mji wa Morogoro jioni ya leo.Kufuatia ushindi huo Rotas atakwenda jijini Dar kupambana na vinara wengine kutoka mikoa mingine katika mpango mzima wa kutimiza kilele cha msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta 2011 ndani ya jiji la Dar,itakayofanyika hapo baadaye.

Pichani kulia ni Rota akishusha mistari yake katika mtindo huru mbele ya hasimu wake Hanstar,katika mtindo ule wa Kubato,wakiwa katika hatua ya mwisho a.k.a fainali,kwamba atakayeshinda ndiye kinara wa msimu wa dhahabu wa unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011 ndani ya mji wa Morogoro jioni ya leo.

Pichani ni Washiriki Wanne kati ya washiriki 44 walioingia nusu fainali katika suala zima la kumsaka mkali wa msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta Freestyle 2011,kutoka kulia ni Rotas,Slim,Ras Q pamoja na Hanstar.
Baadhi ya wakazi wa Morogoro wakifuatilia shindano la Serengeti Fiesta Freestyle 2011 jioni ya leo ndani ya ukumbi wa club ya Four Stars,mjini Morogro.
Pichani ni Vijana wa Morogoro,kushoto ni Goligota pamoja na Ras Q wakionesha umahiri wao wa kubato katika mtindo huru,wakichuana vikali jioni ya leo katika mchakato mzima wa kumpata mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011,ndani ya mji wa Morogoro.

Majaji wa shindano la Serengeti Fiesta Freestyle 2011, Zavara Mponjika pamoja na Squeezer wakijadiliana jambo wakati shindano bado likiwa linaendelea ndani ya ukumbi wa club ya Four Stars,ndani ya mji wa Morogoro.
Picha zaidi nenda kwa Michuzi Jr


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...