Meneja Mafunzo wa Maduka ya Samsung,Paul Kusoga akitoa maelekezo ya namna ya kutumia mashine mpya na yakisasa nchini katika teknolojia ya ufuaji nguo wakati wa kutambulia mashine hiyo kwa waandishi wa habari waliofika leo katika ukumbi wa mikutano wa kampuni ya InterGrated iliyopo Kinondoni Morocco,jijini Dar.
Meneja Mafunzo wa Maduka ya Samsung,Paul Kusoga akimuonyesha Afisa wa Kampuni ya Uwakala wa Matangazo (InterGrated),Laurance Andrew wakati wa kuitangaza mashine mpya na yakisasa kwa ufuaji wa nguo.Kampuni ya Samsung Tanzania leo inatangaza rasmi kuzindua mashine mpya na yakisasa nchini katika teknolojia ya ufuaji nguo yenye lengo la kusaidia kupunguza matumizi ya nishati ya umeme kwa asilimia 70%.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam meneja wa mafunzo na maduka ya Samsung Elekonik katika maduka nchini Tanzania bwana Paul Kusoga alisema kampuni ya Samsung imeamua kuleta mashine hiyo nchini inayotumia Teknolojia ya ECOBUBBLE kutokana na kutambua mahitaji ya watanzania katika kuokoa garama za nishati ya umeme.
Alisema mashine hiyo inauwezo mkubwa wa kutakatisha nguo kwa kutumia nishati ndogo ya umeme kwa wastani wa pungufu wa asilimia 70% sambamba na maji kidogo sana tofauti na ilivyo kwa mashine nyingine za ufuaji nguo.
Mashine hiyo ya kufulia yenye teknolojia ya kipekee ya ecobubble kwa sasa inapatikana katika maduka makubwa nchini, Hii ni fursa ya kipekee kwa wafanya biashara kote nchini kutumia mashine hiyo ili kuweza kupunguza matumizi ya nishati ya umeme na maji ya kufulia.
Alisema mashine hiii pamoja na kuokoa kiwango kikubwa cha nishati na maji lakini pia inauwezo mkubwa wa kusaidia kuongeza ubora wa nguo sambamba na kuwa na programu maalumu ya kufua nguo zenye kutengenezwa kwa kutumia sufi.
Alisema pamoja na mashine hizo kuwa na ubora na faida kubwa ya kuokoa garama za nishati ya Umeme na maji lakini bado zimekuwa na bei nafuu na zinazomfanya mfanyabiashara na watu binafsi kumudu kununua na kutumia kwa muda wote.


Hizo mashine ni za solar au umeme wetu huu huu
ReplyDeleteJe tunaweza kukopeshwa hiyo machine?
ReplyDeleteKweli tujue ni za umeme huu huu au za solar! Maana Hawa TANESCO wanasema wao ni wasambazaji tu wa umeme sio wazalishaji. Inasikitisha kauli kama hiyo ya danganya toto. Kodi Zote wanazochukua, misaada kibao ukiacha rasilimali zilizopo na pesa kwenye mikataba mibovu, lakini hawawezi kuwekeza kwenye nishati mbadala ya JUA au UPEPO! Wanategemea SONGAS tu wazalishe, kwanini wasiwekeze wao pia wawe na sehemu mbali mbali za uzalishaji. Ufisadi mtupu! Wizi Mtupu! Ndio maana mafisadi wengi huingiliwa na majambazi au kuumwa PRESHA au KISUKARI! Laana za mungu hizo. Pesa haramu hazikufikishi mbali, kumbuka kuna mauti, kunakufufuka tena ufanyiwe hesabu siku ya kiyama na uingie motoni! MAFISADI BADILIKENI!
ReplyDeleteMashine ya kufualia ina uwezo wa kuongeza ubora wa nguo? Something fishy here!
ReplyDeleteElectronics Je mafundi ni wakina nani zikiharibika maana wengine hatuishi mjini?
ReplyDeleteJe mkulima naweza kunnuwa pia? maana sisis ndiyo wengi kuliko wafanya biashara.
ReplyDeletebora mdau wa kwanza umeuliza na mimi nauliza kwa sisi tunaokaa pale kimara ambako bomba kuu la maji limepita ila maji mara moja kwa miezi sita sijui hizi mashine zitatufaa maana maji ya kisima yanafanya scum kwa mda mfupi na mwisho wa siku mashine imekufa...daa africa tuna tabu Mungu atusaidie tu katika jina la Yesu.
ReplyDeleteNguo za sufi ama sufu
ReplyDeletewatu wa kimara tatizo la maji mnyika yupo msiwe na wasi aliwaaidi maji mtapata tu
ReplyDelete