
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd,Ziad El Halil akizungumzia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika kampuni hiyo inayotengeneza soda mbalimbali ikiwepo Pepsi,katika halfa ya kuadhimisha miaka 10 ya mafanikio,inayoendelea kufanyika hivi sasa katika viwanja vya Karimjee,jijini Dar.

Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd,Rashid Chenja akitoa hotuba inayoelezea kwa ufupi kampuni ya SBC Tanzania Ltd,wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kampuni hiyo hapa nchini.

Mabosi wakuu wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd,toka kulia ni Mkurugenzi Mkuu,Ziad El Halil,Mkurugenzi wa Pepsi Cola,Rashid Mahmoud,Mwenyekiti wa Bodi,Faisal El Halil,Mtendaji Mkuu wa SBC,Mike Hunter pamoja na Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya SBC Tanzania Ltd,Rashid Chonjo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vyeti vya heshima kwa kuifanikisha kampuni hiyo.hafla hii inaendelea kufanyika hivi sasa katika viwanja vya Karimjee,jijini Dar.

Kamati Kuu iliyofanikisha Hafla ya Miaka 10 ya Kampuni ya SBC Tanzania Ltd ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa mchana huu.
kwa picha zaidi
BOFYA HAPA
kwa picha zaidi
BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...