Dr. Fanuel Shechambo.

Familia ya Marehemu Dr. Fanuel Christopher Shechambo wa Magamba- Lushoto inatoa shukrani za dhati kwa wote walioshiriki katika kumuuguza na hatimaye kutufariji katika msiba wa marehemu baba yetu mpendwa Dr. Fanuel Christopher Shechambo aliyefariki dunia tarehe 16-04-2011 huko Lushoto Tanga na kuzikwa tarehe 19-04-2011 huko kijijini Mlalo-Dule.

Shukrani za pekee tunazitoa kwa Askofu Stephen Munga na uongozi wa KKKT Dayosis ya Kaskazini Mashariki, Mkuu wa chuo Kikuu kishiriki cha Sebasitian Kolowa na wanajumuiya wote wa chuo, Chuo Kikuu cha Tumaini, Hospitali ya KCMC, Hospitali ya Wilaya Lushoto, Hospitali ya Bumbuli, Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), CCM Wilaya ya Lushoto, CHADEMA na CUF, Wabunge wote wa majimbo ya Lushoto, Manispaa ya Ilala, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), KKKT Usharika wa Mlalo, KKKT sharika za Tiku-Lukozi na Magamba, Kanisa la CCT-UDSM, Madrasa ya Mazizini-Lukozi, Majirani wa Dar-es-Salaam, Lushoto na Mlalo pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...