Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), David Minja (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo,baadhi ya tuzo ambazo kampuni hiyo ilizipata nchini Afrika Kusini, baada ya kuibuka washindi wa mauzo, masoko na usambazaji kwa kampuni 16 za SABMiller Afrika.Kushoto ni Meneja Usambazaji wa TBL Kanda ya Kusini, Reginald Mosha.
Maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwa na tuzo mbalimbali ambazo kampuni hiyo ilizipata nchini Afrika Kusini hivi karibuni, baada ya kuibuka washindi wa mauzo, masoko na usambazaji kwa kampuni 16 za SABMiller Afrika.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Rasilimali Watu, Steve Kilindo,Meneja Usambazaji Kanda ya Kusini, Reginald Mosha, Mkurugenzi wa Masoko, David Minja na Meneja Miradi Maalum, Emma Oriyo.
Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Masoko wa Kimataifa,Nick Fell,Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa SABMiller Afrika katika Masoko, Mauzo na Usambazaji, Mark Bowman mara baada ya TBL kupata ushindi huo huko  Johannesburg, Afrika ya Kusini.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla hiyo jijini Johannesburg burg, Afrika Kusini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania, wakifurahia tuzo hizo, wakati wa hafla ya kutoa tuzo iliyofanyika Jahannesburg Afrika Kusini hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...