Kamishna mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya

Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA), imesema makusanyo ya kodi hayajashuka kama inavyodaiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitliya, alisema kuwa makusanyo ya kodi nchini yameongezeka kwa asilimia 18 ikilinganishwa na mwaka uliopita wa fedha. Alisema katika kipindi cha Julai hadi Aprili mwaka huu wamekuwa wakikusanya wastani wa shilingi bilioni 430 kwa kila mwezi.

Alifafanua kiasi hicho ni sawa na asilimia 93 ya makusanyo, ambapo ni pungufu ya asilimia 7 ya malengo yaliyokusidiwa. Alisema mwaka huu wa fedha 2010/2011 wamepanga kukusanya shilingi trilioni 5.24

Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku (sio Nipashe), Zitto alikaririwa akisisitiza kuwa serikali haina fedha na kudokeza kuwa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mapitio ya uchumi ya mwezi Machi mwaka huu, inaonyesha kuwa imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15. Kwamba, Serikali imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15 isipokuwa ushuru wa forodha na hivyo haikufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi.

Hata hivyo, hivi karibuni Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alikanusha vikali taarifa iliyotolewa kwamba Serikali imefilisika na hivyo kulazimika kukopa kutoka benki za ndani ili kugharamia mahitaji ya mishahara kwa watumishi wa serikali pamoja na posho mbalimbali za wabunge.

Mkulo alisema Serikali inalipa watumishi wake mishahara kwa kutumia mapato yake ya ndani na pia ina uwezo wa kugharamia shughuli nyingine pamoja na gharama za kuendesha Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2011

    Watanzania kwa kupenda kujitetea hamjambo. Sasa TRA wenyewe kwenye ripoti yao ya mwaka wameonesha ukusanyaji wa kodi ulipungua kwa sababu ya mgao wa umeme. Taarifa hizo zimewekwa hadharani mnakanusha. Mnaogopa msionekane wazembe. Kama zimeshuka zimeshuka tu. Hazitabadilika kwa kukanusha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2011

    bwana kitilya hilo ongezeko ni nominal tu na si real increase.haliendi sambamba na ukuaji wa uchumi.hiyo tathmini yaki niya wanasiasa na si ya kitaalamu-uchumi.tunaomba ukae kimya kwa kuwa unalijua hilo.zitto ni mwanasiasa na mtaalamu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2011

    TRA nanyi mmezidi ufisadi,yaani mnanuka rushwa hadi kwenye kwapa,kila siku blaa balaa tu mnatupa taabu sana sisi wananchi ku clear mizigo yetu na kudai rushwa na ubadhirifu usio na mwisho,kwa uroho na ubinafsi wenu kiasi kikubwa cha kodi kinapotelea mifukoni mwa wafanya kazi wachache badala ya kwenda serikalini,pia watu wengine huamua kutolea mizigo yao bandari ya Mombasa kuepukana na kero zilizopo hapo Dar,na hii pia inapoteza mapato katika bandari zetu.Wizara husika inabidi ilikazie buti swala hili ingawa limekuwa ni tatizo sugu nchini mwetu.TRA Shame on you !!!!
    mdau Dar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...