Home
Unlabelled
uzinduzi wa NMB bank house leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Je tutafika
ReplyDeleteKaka michuzi naomba uniwekee dukuduku langu ambalo limeniumiza sana na najiuliza hivi je tutafika? Naomba uposi ili wahusika waone na wajifunze kubadilisha jinsi wanavyoendesha biashara zao.
Mimi na mume wangu tuko huku tunasoma na wote tuna scholarships.. Tulivyokuja huku nilijaliwa kupata mtoto. Mwezi wa nne niliamua kumpeleka mtoto kwa wazazi wangu mara moja lakini nilivyokua huku nilikua naangalia ni Bank gani inayotoa huduma nzuri ya foreign account au junior account. Ila zote zinaonyesha ni lazima uwe huko kufungua account hizo. Nilipofika Tanzania kitu cha kwanza nilikimbilia Bank kufungua account kwa vile mtoto tunamwacha nyumbani kwetu hivyo sikutaka account za wazazi wangu wachanganye na zingine walizo nazo kwa vile sisi tuko wengi na kuna wanaowapa hela wazazi na kunawanaochukua hela kutoka kwa wazazi. Hivyo nilitaka kuweka account ya mtoto pekee ili tuweze kuweka hela huku direct za mtoto na wazazi wawe wanachukua kutoka hapo huko Tanzania na account nyingine nilitaka tu iwe ya mtoto hela zake za baadaye..
Yaani vizuizi ni viingi sana visivyo na sababu za msingi kabisa lakini kilichonishangaza mimi ni ile kukataliwa na bank moja kufungua account hizo mpaka nionyeshe work permit ya nchi ninayoishi. Sisi ni wanafunzi na tuna full 100% scholarship. Hela tunayoiweka kwenye mtoto ni ile tunayosave na haturuhusiwi kufanya hata kazi. Sasa wanataka works permit ya nini? Huku niliko tuliweza kufungu bank account zetu kwa kuonyesha tu valid IDs. Nimewaonyesha documents zote lakini bado wakanisumbua kweli na kuniambia kalete hiki kalete kile. Bank nyingine wao wakanisumbua lakini baadaye wakafungua hii account.
Nilivyorudi huku nikawa naongea na rafiki zangu kutoka Kenya na Ghana walishangaa sana sana kwa vile wao kama Ghana wanaweza kufungua account hata online na pia Kenya hata hawaulizi work permit. Na ID wanachukua ya nchi yeyote mradi iwe valid.
Sasa mimi najiuliza Tanzania inasema watu hatuwekezi nyumbani. Tutawekezaje nyumbani wakati biashara zenu mnazifanya kama za miaka ya 70? Kenya kila siku wanaonekana wamepeleka hela nyumbani kwao mabillion lakini ni kwa vile nchi yao imewawekea urahisi wa kufanya hivyo. Sisi kwetu ni vikwazo, vizuizi visivyo na msingi wala nini. Serious hapo Tanzania kuna wahindi wangapi wanaishi bila work permit lakini wana bank account huko India na hata hapo Tanzania pia? Je hamfikirii mambo yenu yamepitwa na wakati na mnapoteza hela nyingi sana kwa kufanya sijui makusudi au mnafikiria mnanikomoa. Kwa vile hata kunishughulikia ilikua kama hawataki vile.. Nimeondoka Tanzania mwaka mmoja na miezi 9 tu lakini kwa vile huduma za huku ni smooth na husumbuliwi niliona kama mauzauza tu. Nikajiuliza mimi nimeondoka muda mchache tu lakini nachanganyikiwa hivi je aliyekaa nje ya nchi zaidi ya miaka mitatu akirudi TZ si atapata kichaa?
Inabidi tubadilike ….Mnakatisha tama sana…
Ni kweli kabisa yote kwani uliyosema nami yamenikumba. Nikiwa Mtanzania na mkazi wa USA kwa miaka mingi sasa, nilichukua kiasi fulani cha fedha kwa nia kuanzisha akaunti na kuzi-deposit ili pia niwe natupia tupia kiasi cha dolla 300-700 kwa mwezi. Lakini huwezi amini ndugu yangu, nilidaiwa vikoro koro vingi mno kiasi kwamba sikuona maana hata kidogo na nikaachana na benki za KiBongo.
ReplyDeleteNakushauri, iwapo utaweza fungua akaunti na Benki ya Kenya hawana mizengwe na waweza kuchukua pesa yako tawi lolote katika nchi yeyote bila ya mizengwe. Benki zetu zinapoteza biashara nyingi mno kwa urasimu usio na tija.
Poleni sana wajameni. Tanzania inatia aibu sana. Mimi ni mfanyakazi katika shirika moja hapo Tz. Ndani ya hilo shirika kuna bank tatu: CRDB, NMB na NBC. Nilitaka kufungua account CRDB, nilisumbuliwa kweli na hivyo vikorokoro. Mara kalete barua ya mwajiri. Mara andika barua ya maombi, mara uwe na marefa watatu wenye account ndani ya hiyo bank. Anyway kwa kuwa niliona ndiyo bank yenye afadhali na iliyosambaa maeneo mengi ya nchi niliamua kutii yale masharti yao. Nilikasirika nikasema hebu niende NBC labda kuna afadhali. Nilichokiona ni yaleyale, tena afadhali hata CRDB. NBC nilikutana na majibu ya kunya kana kwamba nimeenda kuwaibia hela wakati wanategemea account zetu ili waishi.
ReplyDeleteShida ni kwamba Tz utaratibu ukishawekwa hakuna anyefikiria kuufanya uboreke zaidi. Na pia kuna roho mbaya iliyokithiri miongoni mwa wabongo wenzetu.
kipindi kingine nikasafiri kwenda Songea nikamwachia mke wangu Tembo card yangu ili mshara ukitoka aongezee alicho nacho. Bahati mbaya ile kadi ikatumbukia. Mke wangu akajaribu kuomba meneja amtolee. Meneja akamweleza utaratibu kwamba kwa vile kadi haikuwa ya kwako inabidi tuifunge hadi huyo mumeo atakapokuja. Nikawapigia simu wakaniambia niandike fax na details zangu zote. Nikafanya hivyo. Fax ikawafikia mke wangu alivyoenda meneja akamtaka kimapenzi......eti usiponipa sikupi hii kadi. Hata kama ni mumeo. Akamzungusha hadi nilivyorudi ndio akaitoa kwa aibu. Hebu fikirieni watanzania tusivyokuwa serious kwenye biashara. Ni aibu tupu.
Mimi niliwahi kutumiwa hela na kaka yangu toka Italy. Alituma Euro. Zilipofika CRDB pale Morogoro mjini waKwa vile walijua Euro ina thamani kuliko dolakazibadilisha kama USD wakaona nitapata hela nyingi. Niliingia loss ya 1,200,000 TSh. Nilipowanendea nikaambiwa niandike barua niwasilishe shida yangu. Nilifanya hivyo. Nasikitika nilifuatilia hadi nikachoka hakuna fedha ya ziada niliyopewa zaidi ya kupigwa terehe kila nilipokwenda.
ReplyDeleteNatumai NMB umesoma maoni ya wananchi, haijalishi uzuri wa jengo na tawi bali huduma na mawasiliano mazuri.
ReplyDelete