Afisa wa mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom,(Vodacom Foundation) Grace Lyon akifurahia jambo na mwanafunzi wa darasa la kwanza Jamila Hamis wa shule ya msingi ununio iliyopo kata ya kunduchi wilaya Kinondoni jijini Dares Salaam mara baada ya kukabidhi madawadi 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 4,wengine ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Afisa Elimu kata ya kunduchi Geradine Ishengoma ,akiwasisitiza jambo baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio kutunza madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 4 waliyopewa msaada na Vodacom Foundation na kukabidhiwa na Afisa wa mfuko huo Grace Lyon,kulia.
Kutoka kushoto Afisa Elimu kata ya kunduchi Geradine Ishengoma ,Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ununio John Maziku wakiangalia uimara wa moja ya dawati kati ya 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 ,yaliyotolewa msaada na Vodacom kupitia kitengo chake cha Vodacom Foundation,(kulia) aliyekabidhi msaada huo Afisa wa mfuko huo Grace Lyon.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio iliyopo kata ya kunduchi Wilaya ya Kinondoni wakisikiliza jambo kwa umakini kutoka kwa Mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 50 yenye ya zaidi ya Shilingi million 4.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio iliyopo Kata ya Kunduchi wilaya ya Kinondoni jijini Dares Salaam wakifurahia msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Vodacom Foundation yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 na kukabidhiwa na Afisa wa mfuko huo, Grace Lyon hayupo pichani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2011

    Thanks Voda.Wanasomea nje hao??(Utani)..

    Mdau David villa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2011

    Hivi huyu dada (Grace Lyon) hajawahi kusoma Kibosho Girls miaka ya 1997-1998?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2011

    Kumbe Vodacom Foundation kuna vitu vya ukweli ... sio kila siku Mwamvita tu. Hahahaa ni utani tu ... love you Mwamvita wherever you are!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...