Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Shaaban Mwinjaka  (pili kulia) akiwa  ujumbe wa Wawekezaji kutoka nchini Urusi waliomtembelea ofisini kwake. Kushoto ni Bw Aundrey Brazhnik,  Kiongozi wa ujumbe huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Shaaban Mwinjaka
akiwa katika mazungumzo na  ujumbe wa wawekezaji kutoka Urusi waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam asubuhi hii.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Shaaban Mwinjaka amewataka wawekezaji wenye nia njema kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia fursa mbali mbali zilizopo nchini kwa faida na maendeleo ya pande zote mbili.

Dkt Mwinjaka ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, katika mazungumzo mafupi kati yake na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini Urusi wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.

Ujumbe huo wa Wawekezaji kutoka Urusi umeongozwa na Bw Aundrey Brazhnik umekuja nchini ili kufanya mazungumzo na mamlaka mbali mbali kwa lengo la kuwekeza katika miradi ya kuzalisha nishati ya Umeme na uchimbaji wa madini ya aina mbali mbali.

‘Wizara yangu inapenda kuwakaribisha wawekezaji kuja nchini mwetu kushirikiana na Watanzania, tutawapa ushirikiamno wa kutosha ili sote tufaidike na uwekezaji wao ili Taifa na wananchi wake, tufaidike kupitia fursa mbali mbali.’  Amesem,a Dkt Mwinjaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2011

    Uwekezaji katika Madini Mmenichefua. Wananchi tunataka uwekezaji katika viwanda MAMA. Kama ni hivyo tuuze kila mtu kwao ili kila mtu achukue haki yake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2011

    wow! Katibu ni dkt boss ni......??????? Bongo bwana elimu sio ufunguo wa maisha...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...