Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Mh.Sophia Simba akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kliniki ya macho kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iliyo chini ya Shirika linalojihusisha na kuwasaidia watu hao linalofahamika kwa jina la UNDER THE SAME SUN (UTSS) katika makao makuu yake hapa nchini yaliopo Mikochoni Jijini Dar.
Daktari wa Macho kutona nchini Marekani,Dkt. Rebecca Kammer akizungumza na Bw. Elisha Ngeleja ambeye ni mlemavu wa ngozi na mmoja kati ya wafanyakazi wa Shirika la UNDER THE SAME SUN kuhusu uwezo wake wa kuona wakati akiwa katika shughuli zake za kila siku.katikati ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh.Sophia Simba akifuatilia mazungumzo hayo leo katika ofisi za Shirika hilo,jijini Dar.
Dkt. Rebecca Kammer akionyesha namba za kuweza kupima uwezo wa mtu kuona wakati wa uzinduzi wa kliniki ya matibabu ya macho kwa watu wenye ulemavu ngozi.
Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto, Mh.Sophia Simba amuuliza swali mtoto George uwezo wake wa kuona baada ya kuangaliwa macho yake na Dkt. Rebecca Kammer leo.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...