Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi (Mb), atakutana na wasanii katika ukumbi wa BASATA kuanzia tarehe 17 Mei na tarehe 18 Mei, 2011.

Waziri ataongea na wasanii kwa utaratibu ufuatao:-

17/05/2011 (Jumanne) Saa 4:00 asubuhi
Wasanii Wote wa Sanaa za Muziki

18/05/2011 (Jumatano) Saa 4:00 asubuhi
Wasanii Wote wa Sanaa za Ufundi,Filamu na Maonyesho

Izingatiwe kwamba Waziri ataongea na wasanii wa muziki wa aina zote wakiwemo wa Kizazi kipya,Bendi,Disco, Asili,Taarab na kadhalika katika siku ya kwanza.Katika siku ya pili yaani Tarehe 18/05/2011 ataongea na wasanii wa Sanaa za Filamu,Maonyesho na Ufundi pekee.

Wasanii Wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi.

Lengo kuu la mikutano hii kati ya Waziri na Wasanii ni kuongelea maendeleo ya fani za sanaa.

Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...