Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Edith Mushi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwatambulisha wasanii wa muziki kutoka nchini Uganda,Mayanya Douglas a.k.aWease (kushoto) na Ssekibogo Moses a.k.a Radio ambao wataambatana na wasanii wa hapa nchini walioshinda tuzo za Kili Music Awards katika safari yao ya mikoa mitano hapa nchini kutoa shukrani kwa wananchi waliowawezesha kushinda tuzo hizo.Shughuli hii imefanyika mchana huu New Club Maisha,jijini Dar.
Wasanii kutoka nchini Uganga,Mayanya Douglas a.k.aWease (kushoto) na Ssekibogo Moses a.k.a Radio wakiimba moja ya nyimbo zao mbele ya waandishi wa habari na kuahidi kufanya vizuri zaidi hapo kesho kwenye viwanja vya posta,Kijitonyama ambako ndiko itakapozinduliwa rasmi safari ya wasanii hao.
Meneja wa Bendi ya Mapacha Watatu,Hamis Dakota (kati) akiwa na wasanii kutoka nchini Uganda,Wease (shoto) na Radio.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...