Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais. 
Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej.
Na Nafisa Madai – Maelezo Zanzibar

Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais imesema kuwa , kanuni za udhibiti wa bidhaa chakavu na za umeme imeandaliwa kwa lengo la kuweka mazingira safi katika mji wa zanzibar.

Akisoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais kwa mwaka wa fedha 2011/2012,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais,Mhe Fatma Abdulhabib Ferej amesema , kuundwa kwa kanuni hiyo kumetokana na kuzagaa kwa bidhaa hizo ambazo ziko chini ya kiwango kuingizwa kwa wingi hapa nchini .

Amesema sambamba na kuundwa kwa kanuni hiyo wizara yake imekuwa ikifuatilia kwa karibu usimamizi juu ya upigaji marufuku uingizaji na matumizi ya mifuko ya plastic ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa .

Amesema wizara yake pia inasimamia kazi za kupunguza idadi ya kunguru kwa kutumia mitego na sumu ili kufikia lengo la kuangamiza kunguru hapa nchini, ambapo mradi maalum umeandaliwa na utaanza utekelezaji wake katika mwaka ujao wa fedha.

Akizungumzia madawa ya kulevya amesema Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais inachukua juhudi za makusudi za kuongeza kasi ya uwajibikaji wa vyombo vinavyohusika na usimamizi na udhibiti wa dawa za kulevya.

Mhe Fatma amesema mikakati ya kuzuiwa maambukizi mapya ya ukimwi ikiwa ni jukumu la wizara hiyo, imetoa uzito kwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kama wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao, wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili yao pamoja na watumiaji wa madawa ya kulevya kwa njia ya sindano.

Aidha alisema hivi sasa mkakati huo uko katika hatua za mwisho za mapitio licha ya kuchelewa kumalizika mambo ya msingi, katika kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji wake yamefanyika.

Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais katika kufanikisha makadirio na matumizi ya ofisi hiyo imeliomba Baraza la Wawakilishi kuidhinisha juml ya shilingi (bilioni moja mia tano na sabini na tatu milioni) 1,573,000,000. kwa matumizi ya fedha ya mwaka 2011/2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...