Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2011

    Short and clear!

    Sasa Mheshimiwa Zito, Dawa ni kuzikataa kabisa, siyo kuzipangia matumizi yenye maslahi ya kisiasa kama ulivyofanya mwanzo. Tupo pamoja katika mapambano, lakini tuwe na agenda moja tu, ya kuwaendeleza Watanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 11, 2011

    Zitto nakuonea huruma kwani una nia nzuri na maendeleo ya Taifa kuliko ubinafsi lakini uko peke yako. Wenzio hawakuungi mkono na watakuwekea tu uhasama. Labda Slaa angekuwepo bungeni ndiye mtu pekee ambaye angekuunga mkono. Ungekinga tu posho zako kwani hata hao unaowatetea wengine hawana shukrani badala yake wanakudhihaki kwa maneno yao huku kwenye mtandao.
    Mungu akuzidishie.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2011

    Ni uzalendo wa hali ya juu huo. Mtu kukataa posho. Ungepata wabunge wengine wa wanaokuunga mkono, nchi ingepata maendeleo sasa hivi. Lakini kaka upo mwenyewe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2011

    JAMANI MIE PIA BARUA YA KWANZA YA ZITTO KABWE NAIPONGEZA SABABU ANAONESHA NJIA YA NINI BUNGE KWELI LIFANYE KUHUSU PESA ZA NAMNA ILE WANANCHI ZINGEWEKWEZWA PESA KAMA ZILE KWENYE WAKULIMA NA MAFUNDI NA SHULE.

    PIA BARUWA YA MAJIBU KWA MAONI YANGU PIA IMEJIBU VIZURI KAMA MTU UNANIA UKIZIPATA WEWE MWENYEWE PELEKA KULE UNAPOONA UNATAKA ZIPELEKWE ILA NAJUWA KWANINI ZITTO KABWE KATAKA PESA ZIPELEKWE KWENYE CHARITY SABABU HAZIAMINI HIZO PESA KAMA NI PESA ZIMETOKEA KWENYE NJIA NZURI.

    KHALFANI MPEMBA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2011

    R.I.P Amina Chifupa & Chacha Wangwe.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2011

    Haya sasa tuone kweli hizo hela atazipeleka kwa wananchi! alikuwa anataka kutustua moyo tu, Zitto sio tajiri kiasi hicho, bado anahitaji hizo hela.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 11, 2011

    Nakupongeza sana muheshimiwa Kabwe. Mimi binafsi ningependa kukushauri kwamba uirudishe hiyo barua kwa ndugu Nenelwa Mwinambi Wankanga ili akuandikie barua mpya iliyo sahihi na isiyo na makosa. Barua hii uliyopokea inamakosa yafuatayo namba ya simu ilistahili kuandikwa kama ifuatavyo:- +255 222112065-7 ama 0222112065-7 badala ya +255 0222112065-7. Pili namba ya Fax inatakiwa kuandikwa kama ifuatavyo +255 222112538 badala ya +255 0222112538. Na nawaomba wadau wote aware na makosa kama hayo kama kuna mtu asiye amini apige simu kwenye hiyo namba iliyopo kwenye barua yako aone kama anawezapokelewa. Ni hayo tuu mkuu Kabwe warudishie kanyaboya hiyo upate barua halali ndio utuwekee.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2011

    Unajua hii nia nzuri ya Zitto ila hii sio njia nzuri. Hili jambo linakosesha taifa mikakati maalumu ya kimaendeleo. Inatakiwa Mheshiwa Zitto apange mkakati utakaoendeleza KDI hata kama yeye asipotoa posho hiyo. Je, akija mbunge mwingine kwenye jimbo ambaye hana uwezo wa kupeleka hizo posho kwenye KDI ina maana KDI ndio itakuwa mwisho au imekosa mapato sasa itafanyaje? Halafu kuna mipango yeyote kuwa hela hizo hazitaliwa na wajanja wachache zikifika KDI?
    Hii nimeona kwa wabunge wote, utakuta mbunge anatoa shingli millioni moja kuendeleza jimbo bila mikakati maalumu. Tatizo hili litaendelea na halitasaidia taifa. Isiwe jibu ni kumpatia mtu samaki anapoumwa njaa. Inatakiwa tutoe mafunzo au njia ya mtu kuweza kuvua samaki mwenyewe na kujipatia mlo. La sivyo huu mfumo wa kumtegemea mtu mmoja hautaendeleza taifa hata kidogo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2011

    Mungu akutie nguvu school mate wangu Kabwe.Uko peke yako huko bungeni kwasababu wabunge bila posho wanaamini wao sio waheshimiwa.Kuanzia spika hadi mbunge.Pia mheshimiwa Kabwe hilo ni wazo lako hivyo si rahisi wazo kuwa kanuni,tena si rahisi wazo kuwa moyo wa kujitoa. Moyo wa kujitoa unatokana na upendo,na upendo huumbika baada ya kuona au kusikia. Hivyo moyo wako si mioyo ya waheshimiwa hivyo liache kama lilivyo huku ukiende-
    lea kujitoa mwenyewe kwani kutoa si utajiri bali moyo wa huruma na upendo. Huku kwa Obama mambo hayako hivyo, ingawa kipimo ni hicho hicho.

    ReplyDelete
  10. HIVI WATANZANIA IKIFUTWA TU POSHO ZA VIKAO HIZO SHULE KAMA ST MARYS SHULE ZA WATU WENYE PESA JAMANI ZITAKOSA WANAFUNZI.
    PILI WAFANYAKAZI WENGI WATASHINDWA KUWAHUDUMIA NDUGU ZAO MAANA BAADHI YA WAFANYAKAZI WANATEGEMEA HIZO POSHO ILA WAALIMU WATAFURAHI MAANA WAO HAWANAGA POSHO ZA SITTING ALLOWANCE.
    NIMEONA WATU WENGI WANAISHABIA POSHO ISIFUTWA MAANA INAWAUMIZA WANAIPATA KWA SIKU MOJA YAANI MTU UTAFIKIRI TAJIRI WA KAMARI WA DUNIA JAMANI BONGO HATUPENDANI TUFANYE MAANDAMANO YA KUPINGA WAFANYAKAZI KULIPWA POSHO YA KIKAO WAKATI YUPO HAPO HAPO OFISINI NA MUDA WA KAZI ULE ULE NDIO ANATUMIA
    MWACHE WALALAHOI WALIE TU WASIKIE KWENYE RADIO

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2011

    Mh. Kabwe hizo fedha ungetafuta watu waliomasikini katika jimbo lako ukawasaidia, huna haja ya kuonesha umma wewe hutaki hizo pesa. Bali zichukue na kawape masikini. Huko Dodoma tu peke yake kuna watu wa kutosha zitakazowasaidia hizo pesa. Pia kuna jamaa zako wengi huko Kigoma ambao wangefaidika na hizo pesa. Leo ni mbunge kesho ukiukosa hizo pesa utakuja kuzitafuta. Ndio maana Katibu wako alikubali kugombea urais kwa kupitia CHADEMA kwa sharti kuwa alipwe mshahara sawa na mbunge ili kipato chake kisishuke.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2011

    C'mon guys this is just publicity, nothing major. Mimi sio mtalaamu wa kanuni za Bunge lakini sidhani kama Spika ana power ya kusimamisha allowance za wabunge au wafanyakazi wa serikali..

    Kama mheshimiwa Kabwe yuko serious na hii issue why can't he write the bill take it before the parliament. Does it make sense? u bet...However the methodology by the MP here is quite nonsensical...

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 11, 2011

    unajua tunaleta ushbiki bure kabwe amekulahizo posho miaka zaidi ya 7 sasa kama kweli alikuwa azitaki angezikataa toka mwazo ampoteza mvuto toka wameingia wakina mnyika na lisu sasa amebuni njia mpya yakuludisha jina lake nasisi kwa ushabiki tuna msifia lakini kiukweli hana dhamira ya kweli mkibisha ndio tabia zetu lakini subilini mtaona tu MDAU TOKA UJIJI

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 11, 2011

    duh mbona lugha ilotumika kumjibu zito ni kama ya kihuni? yaani haina ustaarabu huwezi amini ni kutoka bungeni ati"ukipokea utaamua uzipeleke wapi?" si wajibu kwa ustaarabu labda kifungu flani section kadhaa kinasema dash dash na ili kukatisha posho inatakiwa ufanye taratibu dash dash au ipitishwe na kifungu dash dash na sio kama hivi inamaanisha ukitaka chukua ukitaka wacha utadhani maskani bwana(mdau uk).

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 12, 2011

    Mabepari walia, mabepari walia.
    Utajili wa mirija
    Walipotangaziwa, walipotangaziwa
    Azimio la Arusha.

    Mafisadi walia, mafisadi walia
    Uongozi wa dhuruma
    Walipotangaziwa, walipotangaziwa
    Kupunguziwa posho.

    Wabunge wanakula, Wabunge wanasaza
    Raia twafa njaa
    Walipotangaziwa, walipotangaziwa
    Kushusha mishahara.

    Wabunge wanakunywa, wabunge wanamwaga
    Raia tuna kiu
    Walipotangaziwa, walipotangaziwa
    Kuuenzi uzalendo.

    Wabunge wanavuta, wabunge wamekinai
    Raia hatujaliwi
    Walipotangaziwa, walipotangaziwa
    Kutenda yaliyomema.

    Nyerere tusikie, Baba tusikie
    Kilio chetu watoto
    Walipotangaziwa, walipotangaziwa
    Miiko ya uongozi.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 12, 2011

    Maombi ya Zito si mabaya ni mfano wa kuigwa na wabunge wote - je kama kila mbunge akaamua kujitolea kama hivyo tu; hata negativity mind ya watu wengi kuhusu wabunge itabadilika. Ofisi ya bunge inatakiwa iwahamasishe na kusaidia fikra hizi - hii ni just simple transfer payment na kuna ushahidi wa ombi toka kwa mbunge mwenyewe; why tuna-complicate even do-able simple things! Kama angekuwa ni mzungu basi ingekuwa yes sir will do that immediatelly! Come'on Watanzania lets start thinking progressive!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 12, 2011

    Nafikiri Watanzania mnakosea sana kumkejeli Kabwe. Anony hapo juu umesema anatakiwa azichukue akawape maskini. Anony mwingine kasema hizo pesa ndio zinategemewa na ndugu wa waheshimiwa. Basi wooote naona hamjui kanuni za maendeleo. Kimsingi maendeleo yanatakiwa yamfaidishe kila mtu atafute mwenyewe na apate. Na ili iwe hivyo ni lazima pesa zielekezwe kwenye maendeleo ili kila atakayefanya kazi kwa bidii azipate kutokana na kazi yake na sio kwenye mifuko ya watu wachache. Kulimbikizia wabunge posho nyingi manake pesa zikosekane kwenye mambo ya maeendeleo. Je kama Mbunge akiamua asiwape hao ndugu? Je akiamua anunue gari lake la kifahari wewe unayezisubiri utazipata? Na pia mambo kama hayo yanaendelea kkufanya watu wengine wawe wanyonge kwa watu wanaowategemea wakati wapo pia wanafanya kazi ila tu ni mifumo mibaya inayowafanya wasifaidike na jitihada zao.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 12, 2011

    HIVI WAHISANI WAKO WAPI JAMANI TUNAOMBA WAINGILIE KATI KWANI BILA HAO SAUTI YA UMMA HAINA NGUVU TANZANIA.TAFADHARI TUNAOMBA MSAADA WAHISANI WATUSAIDIE KWA HILO KWANI WANA NAFASI KUBWA KULIKO HATA SISI WALALA HOI

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 12, 2011

    Tehee hee heee. Hii ni kuhakikisha kwamba kila mtu anahesabika kwamba amekula posho.

    Hii move ni nzuri sana kisiasa. Sasa hivi imani ya wananchi kwa wabunge wa chama twawala inazidi kushuka kwa sababu wao ndio wapo mstari wa mbele kung'ang'ania posho. Kama posho ikishuka wabunge wa chama twawala watakuwa wakali zaidi kwa serikali yao. Kama ikibaki hivyo hivyo wananchi tutakuwa wakali zaidi kwa wabunge wa chama twawala.

    Mikakati ya uchakachuzi inabidi ianze sasa la sivyo CCM wajiandae kuwa chama cha upinzani uchaguzi ujao.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 12, 2011

    Kwa nini barua kwa mtu binafsi iletwe kwa jamii (in public)?
    Kabla ya kujibu soma tena swali!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 12, 2011

    ni unafiki mtupu tu kutaka kuwaonyesha watanzania kuwa eti yeye ana usongo na matatizo ya watu wake.Kwa nini asitangaze kimyakimya azipeleke huko mwenyewe humu mitandaoni anamuonyesha nani ukasrimu huo???

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 13, 2011

    Viva Zito kabwe! Kama kila mbunge angetengeneza charity jimbioni mwake! afu hivzo pesa zikawa zinanenda huko, maendeleo yangekuwa so fast!

    Mishahara tu inawatosha milioni 9 kwa mwezi, hasa posho za nini tena bora ziende jimboni nzaikafanye kazi!

    Safi sana zito! Wengine nao waige ! tulete maendeleo faster!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 13, 2011

    huu ni unafiki tu kama kweli wana nia ya dhati wangepeleka hoja binafsi bungeni na kufuata taratibu zinazokubalika ..kwani spika hana uwezo wa kubadilisha sheria kwa kuandikiwa barua na mbunge....huu ndio unafiki ambao umenifanya nianze kupata wasiwasi juu ya chama cha zito na wenzake maana hoja zao zote ukiangalia ni za kutafutia umaarufu wa umma hasa umma usiojua sheria .....

    mdau mwenye akili

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 15, 2011

    Je ni kweli Zitto anataka kuwasaidia wananchi wa jimbo lake? Kama ni hivyo kwa nini asianze na zile millioni 90,000/= (milioni tisini ) alizosaini, kuzikubali na kuzichukua yeye mwenyewe kama mkopo wa gari la mbunge kisha akazipeleka zote huko atakako kisha akawa anakatwa yeye kidogo kidogo? Zile hazikuwa na sheria wala kanuni ni hiyari ya kila Mbunge, mbona alizichukua na akakaa kimya? asitake sifa tu na zile kachukua!!!!!!. CHADEMA Waanze kupunguza posho za vikao wanazopeana wao wenyewe wakikutana, mbona zile wanachukua na hawasemi wanadhani hatujui? Slaa alipoenda kugombea urais, alijua hata pata na kabala ya kwenda aliwapa CHADEMA masharti kuwa kama hato pata wamlipe milioni 7.5 kila mwezi. Zito huoni kama unaramba matapishi yako mwenyewe??????????? Anzisha jingine tuko nyuma yako, tutakuunga mkono.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...