Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake katika Mkutano wa Mataifa ya Tropiki yaliyo katika Ukanda wenye Misitu mikubwa na yenye kuvuna mvua kwa wingi, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo Brazzaville jana Ijumaa Juni 3.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo jijini Brazzaville, jana Ijumaa, Juni 3, 2011 kuhudhuria Mkutano wa 3 wa Nchi za Tropiki zilizo katika ukanda wenye misitu mikubwa na mvua nyingi. Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka katika nchi zaidi ya 30 zilizo katika ukanda huo, mataifa yaliyoalikwa sambamba na mashirika ya Kimataifa yanayoshughulika na masuala ya mazingira.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya marais wa nchi mbalimbali katika mkutano wa Mataifa ya Tropiki yaliyo katika Ukanda wenye Misitu mikubwa na yenye kuvuna mvua kwa wingi, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo Brazzaville jana Ijumaa Juni 3.
Kutoka (kushoto) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Waziri katika ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Fereji na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, wakiwa katika mkutano huo, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya watu wa Kongo Brazzaville, jana Ijumaa Juni 3. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.


kweli congo wapo juu angalia hiyo taswila utajionea jinsi kunavyopendeza pamoja na shida za mapigano yaliyopo nchini humo
ReplyDeletebongo tupo huru na amani lakini mazingira kwishinei
kabla ya kusoma nilidhani hapa ni nje ya Afrika.Afu mnaita Dar kama NY angalia hii mandhari ya hii sehemu ilivyo?Tukirudi tunabaki kuhadithiana eeh bwana ule mji umejengwa kiutalaam. Hakuna kiongozi wa Tz aliyewahi kuomba misaada ili ajenge architechs kama hii(atleast moja) .Instead viongozi wanaomba misaada isiyokuwa na kichwa wala miguu na kuongea blah blah blah kibao
ReplyDeleteUncle huyo anaesoma gazeti picha ya nne anasoma kweli,mh mbona gazeti lipo kichwa chini miguu juu.
ReplyDeleteHuyo mheshimiwa ktk picha ya nne anasoma hiyo newspaper upside down au ni macho yangu???
ReplyDeleteheheheh jamani hiyo picha ya nne huyo anayesoma kitabu kakigeuza au MACHO yangu ? wadau nisaidieni heheheheh uuuuwwwiiiiiii
ReplyDeleteKongo Brazaville inaonyesha kuwa ni kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu!
ReplyDeleteKabila anapiga nondo adi noma. Sio viongozi wengine vitambi vitambi !
ReplyDeletemdau paris
wadau vipi Jeografia imewapiga chenga!, hii sio DRC kwa Kabila, huku ni Congo-brazzavile (Repabliki ya Congo) kwa Raisi Denis Sassou Ngueso, Raia wake ni takribani milion 4 tu. Wana mafuta hao na GDP yao ni kama US$ 5,000 ukilinganisha na bongo TZ kwetu US$ 600 hivi. Dini 99.1% ni wakristo mbalimbali. Hawana vita hao, vita viko DRC kwa Kabila ila serikari yao ni kama ya kidictator kama vile ilivyokuwa Misri, Uganda, Sudan.
ReplyDeleteNa pia lugha ya Congo ni Kifaransa tu, jarida analosoma huyo yamaa limeandikwa upande mmoja habari kwa Kifaransa, upande mwingine kwa kiingereza, hivyo kava la nje mnaloliona juu chini ni kawaida, litaonekana juu chini. Wenye hisa DCB, Twiga, Tanga angalieni ripoti zenu za mwaka ziko hivyo hivyo upande mmoja kiswahili upande mwingine kiingereza na kava la juu lazima upande uonekane juu chini.(kumradhi kiswahili)
alex bura, dar