Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu huria nchini wa kituo cha Bukoba wakijaribu kusoma soma muda mfupi kabla ya kuingia kwenye vyumba vya mtihani kufanya mitihani yao ya kumaliza mwaka wa masomo 2010/2011, mtihani huo ulianza jana na unafanyika kwenye jengo jipya la chuo hicho lililoko barabara ya kashozi iliyoko katika manispaa ya Bukoba. Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii, Bukoba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2011

    mandhari nzuri ya kujisomea, yaani nyie acha mimi sijafika huko bukoba au Mwanza lakini jinsi ninavyoona majabali yananivutia sana. Mimi sijui kwa nini wanahama kwao kuzuri namna wanakuja Dar kwenye misongamano na joto.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2011

    Kisomo ni kitu cha maana, hata usome chini ya jiwe ili mradi elimu. Hii ndio tunatakiwa kutangaza tanzania. Elimu, elimu, elimu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2011

    Hapo mpaka ukute sehemu imeandikwa "NO SCHOOL AHEAD" ndo unachana na mambo ya shule

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2011

    Hapo zamani Bosi fulani kutoka Kanyigo alitaka kujenga hoteli miaka ya 85 hivi sijui kilitokea nini mpaka sasa ndo kama ilivyo hivyo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2011

    Nami nilisoma BA huko Open univ, na kutumisa sana Teknohama na kujiwekea nidhamu ya kusoma kila wiki. Shule ya OUT inapanua uwezo wa kuchanganua mambo na kuelewa mambo mengi sana. Nimesoma Masters Univ of London, UK, na ilikuwa kama kumsukuma mlevi kutokana na uzoefu wa kudima Open. Kazeni buti, shule ya Open Univ iko juu sana
    Mdau
    zenj

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2011

    Safi sana hasa kwa kutambua ile BIASHARA haina nafasi tena katika dunia hii

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2011

    Wewe anonymous wa 04:46:00 unatafuta uchokozi wewe; utani wa ngumi huo. Biashara ipi hiyo unaongelea hapa? Mh;haya wee.Naamini wenyewe wamepata ujumbe. Tunawatakia mtihani mwema wadau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...