Jumuia ya wanafunzi waliowai kusoma na ambao wanasoma katika shule ya Secondari ya Makongo, wanatarajiwa kufanya Bonanza la aina yake katika viwanja vya Leders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam..
Dhumuni la Bonanza hilo ni kuhamasisha vijana kwa wazee kuwa michezo ni ajira.,Makongo ni moja ya shule ambayo imetoa wanamichezo wengi ambao wamefanya mengi katika sekta ya michezo mbali mbali hapa nchini..
Ratiba kamili ya bonanza hilo ambalo,lifanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Leders club watu wote wapenda michezo wataalikwa kuja kushiriki katika tamasha hilo,ambapo kingilio kitakuwa shilingi 2000 tu kwa kila mtu.
RATIBA NI KAMA IFUATAVYO
08:00 - 09:00 Asubuhi -Wanafunzi waliosoma na walioko Makongo watajumuika kwa pamoja kufanya Usafi katika eneo lote la shule ya Makongo.
09:00 - 10:00 Dua au Misa kwa ajili ya kuwaombea Walimu na Wanafunzi wote waliosoma Makongo Ambao Wametutangulia mbele za haki.
10:00 - 11:00 Watu wote kutoka katika Shule ya Makongo kuelekea katika Viwanja vya Leders Club Kujumuika kwa pamoja na wadau na wapenzi wa michezo hapa Nchini.
11:00 - 14 : 00 Michezo mbali mbali kuanza,kwa wanafunzi wote, waliosoma na wanaoendelea kusoma Katika shule ya Makongo pamoja na wadau wa michezo kujumuika kwa pamoja.
14:00 - 14 :30 Lisala kwa wanafunzi kwenda Waalimu na Uongozi wa Shule na Lisala kwa wanafunzi wa Zamani kwenda walimu na wanafunzi wa sasa.
16:00 - 18:00 Mechi kati ya wanafunzi wa Makongo na Timu ya Yanga
18:00 - 00:00 Burudani Kutoka kwa Tmk Wanaume,Chege Na Temba,Mapacha wa Tatu,Dogo Janja na Tip Top Connection,Na wengine wengi Kutoka Makongo.



Hii nembo inaonesha waliosoma makongo ni wazungu...strange idea!
ReplyDeleteHalafu siyo waliosoma bali aliyesoma kwani FSM imefupisha maneno Former "Student" of Makongo na siyo Former "Students" of Makongo.Inakuwaje jumuiya ya mtu mmoja!Yaweza kuwa mzungu mmoja aliyesoma Makongo.Kazi tunayo!!!.
ReplyDeleteKwa mwendo huu wa kutojithamini hatutoki!
ReplyDeletebadilisheni hiyo nembo haifai strange idea kweli kweli
ReplyDelete