
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampini ya utengenezaji madawa ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES,Mercy Marealle akimkabidhi gari aina ya Toyota Nadia,Riyaz Gangji ambae ni mshindi wa manunuzi ya Dawa zinazotengenezwa na kampuni hiyo kwa mwaka 2010.
Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES,Flora Kessy akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) namna walivyoweza kuendesha droo ya kumpata mshindi wa manunuzi ya dawa leo katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya kampuni hiyo,Keko jijini Dar.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampini ya KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES,Mercy Marealle na kulia ni Meneja wa IT na Mauzo wa kampuni hiyo,Alfonce Macha.
Mshindi wa Gari aina ya Nadia kutoka kampuni ya Abbas Emporium,Riyaz Gangji akizumza na vyombo vya habari juu ya ushindi alioupata leo.kulia ni Mwanae Riyaz akiwa ni mwenye furaha baada ya baba yake kushinda gari hilo.




KEKO PHARMACEUTICAL INDUSTRIES (1997) LIMITED leo wametoa rasmi zawadi ya gari aina ya Toyota Nadia kwa mshindi wa manunuzi kwa mwaka 2010.
Kuanzia January Mwaka 2010, Kampuni iliamua kuendesha promosheni ya kuongeza mauzo ya dawa ya kupunguza maumivu ijulikanayo kama Diodol ili kushindana na dawa nyingine za aina hiyo zilizopo sokoni.
Mchakato huo ulihusisha wasambazaji wake waliopo jijini Dar es salaam na mikoani kwa ujumla ambapo walipangiwa malengo ambayo yalikuwa na zawadi kama yakifikiwa.
Kati ya Wateja wetu wote Kampuni ya Abbas Emporium ndio iliyovuka lengo la manunuzi kwa kuuza dawa ya Maumivu Diodol ya Vidonge vya 500mg. Kampuni imeona ni vyema imkabidhi zawadi ya Gari aina ya Toyota Nadia, lenye dhamani ya 12,000,000 ( Milioni Kumi na Mbili Tu) Kama motisha kwa jitihada zake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...