Marehemu Prof. Haroub Othman enzi za uhai wake
Ndugu yangu Michuzi Habari za masiku. 
Nilikuwa nakuomba uwaarifu ndugu, jamaa na marafiki kuwa leo tunatimiza miaka miwili toka mzee wetu Haroub Othman atutoke.
 Tutakuwa na kisomo siku ya Alhamis Msikiti Ngazija, mtaa wa Sewa na India saa 11 jioni kwa wale watakaokuwa na muda tutaomba mfike biba kukosa na kina mama nao pia wanakaribishwa. Ningependa pia kuwaomba waendelee kumuombea Mola amfungulie pepo na wasiache kufuata yale mema aliyokuwa akiyatenda wakati wa uhai wake.
Natanguliza shukurani.

Tahir

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2011

    We miss you our lovely Prof. Busara na hekima zako hatutazisahau kamwe. Ulikuwa baba na kiongozi wa wengi.
    Mungu aendelee kuwafariji familia yake, nanyi mzidi kutunza na kuenzi Hekima na Busara zake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2011

    Poleni sana. Marehemu alinifundisha. Mambo ya Nicaragua na harakati za Sandinista na Contra. Nikikumbuka hayo namkumbuka marehemu. Great scholar. Mola amlaze pema peponi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2011

    Mola amlaze mahala pema peponi. Ila nina swali kwa huyo mtoa taarifa, kwani kina mama siyo sehemu ya hao walioalikwa mwanzo? Hiyo sentensi ya KINA MAMA NAO WANAKARIBISHWA, nadhani haikutakiwa kuwepo. Maana hapa mtoa taarifa anaonesha kuwa ni mdhalilishaji wa jinsia ya kike ile mbaya.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2011

    Anon wa hapo juu...Ulianza vizuri na swala , lakini bila kusubiri jibu, kutoka kwa mtoa taarifa uliendelea kukosoa . Ungelimjua mtoa taarifa hii usinge hata siku moja dai kwamba ni mdhalilishaji wa jinsia...Kutokana na hulka zetu mara nyingi shughuli za kisomo kama hiki huwa msikitini kwa kina baba na kina mama huwa na kisomo chao nyumbani...kwa hiyo mtoa taarifa akiwa pia ni Mtoto pekee wa marehemu amejumuisha jinsia zote pamoja msikitini, Hapo utaona jinsi ya tofauti yangu na yako, kwani mimi nampongeza kwa matayarisho hayo...
    Badala ya kutoa Dua kwa Mzee wetu inabidi kurekebishana na wanaojifanya kujua kuliko wengine...mungu amlaze mahali pema na awape subira wanaadamu wengine ili tuishi katika ulimwengu wa heshima na amani kama alivyoishi na kutufundisha, Prof!
    @ TAHIR,Ingawa tupo mbali , mioyo na dua zetu zipo pamoja nanyi....

    MDAU... CANADA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...