Hayati Mwashabani A Liganja
BISMILLAH RAHMAN RAHIM
Mpendwa Mama,
Ni miaka minne (4) sasa tangu tulipopokea msiba wako kwa machungu mengi. Daima tunamshukuru Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi, si tu kuwa Mama mwenye upendo bali kwa kuwa ulikuwa mtu wa pekee miongoni mwetu.
Ulibarikiwa kwa mambo mengi, ucheshi, hekima, zaidi sana sauti iliyobeba matumaini siku zote. Na juu ya yote kufanya kila jambo kwa kusudi maalum.
Daima unakumbukwa sana na Mumeo Mpenzi George Mapango,
wanao Mariam (Chuma), Eva (Hawa), Jackson (Kibabu), Patrick (Saidi), Rose, Richard na mziwanda wako Maria uliyependa kumuita IA. Wakwe zako Deogratias Sakawa, Ibrahim Lugandu, wajukuu zako Precious (P), Pricilla, wadogo zako, ndugu, jamaa, Marafiki zako, Majirani na Wafanyakazi Wenzako.
Tutaendelea kufuata ushauri wako na mema mengi uliyotufundisha. Kwa upendo wako unatuunganisha Familia na tutaendelea kukumbuka busara zako.
KISOMO TAREHE 07 JUNI, 2011 SAA 10:00 JIONI
NYUMBANI KWAKE OCEAN ROAD FLATS .
INNA LILLAHIAHI WA INNA ILAYHI RAJI’UN



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...