Salamu Kaka Issa,

Matumaini yangu u mzima na unaliendeleza libeneke la habari mtandaoni.

Kaka naomba utusaidia kutangaza utangaze jipya la udalali wa nyumba na viwanja na maofisi mtandaoni ambalo linapatikana kupitiawww.mydalali.com.

Watu wengi wamechoshwa na udanganyifu wa madalali wa mitaani ndio maana tumeona tujaribu kusolve hili tatizo kwa kufanya udalali mtandaoni.Mpangaji au mnunuzi ataiona nyumba na bei yake  kwahiyo atafanya uamuzi popote pale alipo.

Kwa watafutaji wa nyumba za kupangisha au kununua na wanaotafuta viwanja wanaweza kupata habari kupitia mtandao huu na kama anaihitaji nyumba ya aina fulani anaweza kutuma details na akasaidiwa kutafuta nyumba ya aina hiyo. Pia kwa wanaomiliki nyumba au ardhi na wanataka kuiuza wanaweza kuingia kwenye mtandao na kututafuta na tukaiweka nyumba au ardhi au ofisi na wateja wakaiona mtandaoni.

House or plots for sale,House or apartments for rent...Its a platform where the landlords and tenants meet and we are trying to minimize the cost and time spent on looking for land or a house.

Asante Kaka Michuzi na naamini utatusaidia kwenye hili na utafanya jamii yote ya wanamtandao na wana wa libeneke la Michuzi kufahamu.

Natanguliza shukrani zangu.

Wasalaam,

William Jackson.

www.mydalali.com  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    What a nice surprise!. Kwa mara ya kwanza naona nyumba na viwanja kwa bei ya kibinadamu. Mara nyingi, bei ktk site za bongo, zinakuwa katika malaki ya pesa ya Kimarekani na zinazidi hata bei za nyumba za sehemu kama Lauderdale, Fl.
    Keep it up na watu watajivuta kwako
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    Shida ni kuwa hizi site za Real Estate hazidumu na haziwi updated. Utaona zinaanza hivi ila kila siku ukienda mwaka mzima site iko vile vile, hakuna nyumba mpya, haionyeshi zilizouzwa haionyeshi viwanja vipya na most of the tabs don't even have any information. Nimeshachoshwa na site za Real Estate za bongo. Hebu kama mnaamua kufanya biashara jaribuni kuwa waungwana siyo unauza kiwanja kimoja halafu unasahau site maana umepata ka-commission.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...